A mulher virtuosa
A mulher virtuosa de Provérbios 31 é um retrato de excelência. Seu valor excede o de rubis — ela é sábia, trabalhadora, generosa e teme ao Senhor acima de tudo.
Uma joia rara
Mulher virtuosa, quem a achará? Seu valor excede o de rubis. Ela é o coração da família e a força do lar.
Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata?
Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani.
Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata?
Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani.
Mume wake anamwamini kikamilifu,
wala hakosi kitu chochote cha thamani.
Humtendea mumewe mema, wala si mabaya,
siku zote za maisha yake.
Huchagua sufu na kitani,
naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii.
Yeye ni kama meli za biashara,
akileta chakula chake kutoka mbali.
Yeye huamka kukiwa bado giza,
naye huwapa jamaa yake chakula
na wajakazi wake mafungu yao.
Huangalia shamba na kulinunua;
kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu.
Hufanya kazi zake kwa nguvu,
mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake.
Huona kwamba biashara yake ina faida,
wala taa yake haizimiki usiku.
Huweka mikono yake kwenye pia,
navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi.
Huwanyooshea maskini mikono yake
na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.
Mke mwenye tabia nzuri ni taji la mumewe,
bali aaibishaye ni kama uozo
katika mifupa ya mumewe.
Sasa, binti yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba. Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri.
Caráter acima da aparência
Enganosa é a graça e vã é a formosura, mas a mulher que teme ao Senhor será louvada. A verdadeira beleza é interior.
Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu,
na uzuri unapita upesi;
bali mwanamke anayemcha Mwenyezi Mungu atasifiwa.
Vivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, bali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.
Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake,
bali mpumbavu huibomoa nyumba yake
kwa mikono yake mwenyewe.
Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi,
bali mke mwenye busara hutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Vivyo hivyo, wafundishe wanawake wazee kuwa na mwenendo wa utakatifu, wala wasiwe wasingiziaji au walevi, bali wafundishe yale yaliyo mema, ili waweze kuwafundisha wanawake vijana kuwa na kiasi, wawapende waume zao na kuwapenda watoto wao, wawe waaminifu, watakatifu, wakitunza vyema nyumba zao, wema, watiifu kwa waume zao, ili mtu yeyote asije akalikufuru neno la Mungu.