Não temas
'Não temas' é uma das frases mais repetidas na Bíblia. Deus a pronuncia nos momentos de maior temor, lembrando que sua presença e poder são maiores que qualquer ameaça.
Deus está contigo
Não temas, porque eu sou contigo. Deus repete essa promessa em cada crise, guerra e desafio que seus filhos enfrentam.
Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;
usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.
Nitakutia nguvu na kukusaidia;
nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Kwa maana Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako,
nikushikaye mkono wako wa kuume
na kukuambia, Usiwe na hofu,
nitakusaidia.
Usiogope, ee Yakobo uliye mdudu,
ee Israeli uliye mdogo,
kwa kuwa Mimi mwenyewe nitakusaidia,"
asema Mwenyezi Mungu,
Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Wewe uletaye habari njema Sayuni,
panda juu ya mlima mrefu.
Wewe uletaye habari njema Yerusalemu,
paza sauti yako, piga kelele kwa nguvu,
paza sauti, usiogope;
iambie miji ya Yuda,
"Yuko hapa Mungu wenu!"
Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuwa pamoja nawe popote utakapoenda."
Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anaenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi."
Baada ya jambo hili, neno la Mwenyezi Mungu likamjia Abramu katika maono, akaambiwa:
"Usiogope, Abramu.
Mimi ni ngao yako,
na thawabu yako kubwa sana."
Coragem diante do perigo
Não tenhas medo — o Senhor teu Deus está no meio de ti, poderoso para salvar. Ele luta por nós e dá forças aos medrosos.
Katika siku hiyo watauambia Yerusalemu,
"Usiogope, ee Sayuni;
usiiache mikono yako ilegee.
Mwenyezi Mungu, Mungu wako, yu pamoja nawe,
yeye ni Shujaa mwenye nguvu anayeokoa.
Atakufurahia kwa furaha kubwa,
atakutuliza kwa pendo lake,
atakufurahia kwa kuimba."
Nabii akajibu, "Usiogope. Wale walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao."
Kisha Al-Yasa akaomba, "Ee Mwenyezi Mungu, mfumbue macho huyu mtumishi ili apate kuona." Ndipo Mwenyezi Mungu akayafumbua macho ya yule mtumishi, naye akatazama na kuona vilima vimejaa farasi na magari ya vita yaliyowaka moto yamemzunguka Al-Yasa pande zote.
Usiogope, ee nchi;
furahi na kushangilia.
Hakika Mwenyezi Mungu ametenda mambo makubwa.
Lakini Mwenyezi Mungu akaniambia, "Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza. Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe," asema Mwenyezi Mungu.
Usiku mmoja Bwana Isa akamwambia Paulo katika maono, "Usiogope, lakini endelea kusema wala usinyamaze, kwa maana mimi niko pamoja nawe, wala hakuna mtu atakayeweza kukushambulia ili kukudhuru, kwa kuwa nina watu wengi katika mji huu."
Nawe mwanadamu, usiwaogope wao wala maneno yao. Usiogope, ijapo michongoma na miiba vinakuzunguka na unaishi katikati ya nge. Usiogope yale wasemayo wala usitishwe nao, ijapo wao ni nyumba ya uasi. Lazima uwaambie maneno yangu, ikiwa watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni waasi.
Fé que vence o medo
O medo não vem de Deus. Jesus disse: não temas, crê somente! A fé dissipa o medo e nos conecta ao poder de Deus.
Aliposikia hayo waliyosema, Isa akamwambia huyo kiongozi wa sinagogi, "Usiogope. Amini tu."
Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia ibilisi atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji la uzima.
Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika Jehanamu.
Lakini alipokuwa akifikiri kufanya jambo hili, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea katika ndoto na kusema, "Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho wa Mungu.
Ndipo malaika akamwambia, "Usiogope, Mariamu; umepata kibali kwa Mungu.
Simoni Petro alipoona haya yaliyotukia, alianguka miguuni pa Isa na kumwambia, "Bwana, ondoka kwangu. Mimi ni mtu mwenye dhambi!"