Órfãos
Deus tem um cuidado especial pelos órfãos. Ele se apresenta como pai dos que não têm pai e defensor dos desamparados, e ordena a seu povo que faça o mesmo.
Deus, pai dos órfãos
O Senhor é pai dos órfãos e protetor das viúvas. Ele sustenta os que perderam amparo humano e cuida deles com ternura.
Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake,
mtukuzeni yeye anayepita juu ya mawingu:
jina lake ni Mwenyezi Mungu,
furahini mbele zake.
Baba wa yatima, mtetezi wa wajane,
ni Mungu katika makao yake matakatifu.
Mwenyezi Mungu huwalinda wageni
na kuwategemeza yatima na wajane,
lakini hupinga njia za waovu.
Teteeni wanyonge na yatima,
tunzeni haki za maskini na waliodhulumiwa.
Sitawaacha ninyi yatima; nitakuja kwenu.
O chamado da justiça
A religião pura é visitar órfãos e viúvas em suas aflições. Deus ordena a defesa do necessitado e o cuidado com os mais frágeis.
Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu, Baba yetu, ndiyo hii: ni kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.
Jifunzeni kutenda mema, tafuteni haki.
Wateteeni waliodhulumiwa.
Teteeni shauri la yatima,
wateteeni wajane.
"Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Fanyeni hukumu za haki, onesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi. Msimdhulumu mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’
"Usimdhulumu mjane wala yatima. Ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao. Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima.
kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada,
naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.
Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki,
nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.