Palavras de conforto
Deus é o Deus de todo conforto. Ele consola os que choram, restaura os quebrantados e promete que a dor presente dará lugar à alegria eterna.
O Deus de toda consolação
Bendito seja o Deus e Pai de nosso Senhor Jesus Cristo, Pai das misericórdias e Deus de toda consolação, que nos consola em todas as tribulações.
Mungu wa faraja yote
Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu.
Mungu wa faraja yote
Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu. Kama vile mateso ya Al-Masihi yanavyozidi maishani mwetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kupitia kwa Al-Masihi. Ikiwa tunataabika, ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu; tukifarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu, iwaleteayo saburi ya mateso yale yale yanayotupata. Nalo tumaini letu kwenu ni thabiti, kwa sababu tunajua kwamba kama vile mnavyoshiriki mateso yetu, ndivyo pia mnavyoshiriki faraja yetu.
Kama vile mateso ya Al-Masihi yanavyozidi maishani mwetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kupitia kwa Al-Masihi.
Kwa maana hakupuuza wala kudharau
mateso ya aliyeteswa;
hakumficha uso wake
bali alisikiliza kilio chake.
Mwenyezi Mungu yu karibu na waliovunjika moyo,
na huwaokoa waliopondeka roho.
Promessas de restauração
Deus sarará o quebrantado de coração e atará as suas feridas. Quem semeia em lágrimas, colherá com júbilo.
Anawaponya waliovunjika mioyo
na kuvifunga vidonda vyao.
Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,
bali upendo wake hudumu siku zote.
Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,
lakini furaha huja asubuhi.
Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
Mtwike Mwenyezi Mungu fadhaa zako,
naye atakutegemeza,
hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
Andika maombolezo yangu;
andika machozi yangu katika kitabu chako:
je, haya hayapo katika kumbukumbu zako?
Mwenyezi Mungu ni kimbilio la wanaodhulumiwa,
ni ngome imara wakati wa shida.
Mwenyezi Mungu ni mwamba wangu,
ngome yangu na mwokozi wangu;
Mungu wangu ni mwamba wangu,
ninayemkimbilia.
Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu,
ngome yangu.
Paz e descanso
Jesus disse: 'Vinde a mim, todos os cansados e sobrecarregados, e eu vos aliviarei.' A paz de Deus que excede todo entendimento guarda o coração.
Isa awaita waliolemewa na mizigo
"Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Isa awaita waliolemewa na mizigo
"Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha katika nafsi zenu.
Heri wale wanaohuzunika,
maana hao watafarijiwa.
Amani nawaachia; amani yangu nawapa. Amani hii ninayowapa si kama ile ulimwengu unatoa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.
"Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu."
Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.
Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Al-Masihi Isa.
Esperança eterna
Deus enxugará toda lágrima. A dor presente é momentânea, mas a glória futura é eterna. O Senhor transforma luto em dança.
Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, "Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita."
Naye yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi akasema, "Tazama, nayafanya mambo yote kuwa mapya!" Kisha akasema, "Andika haya, maana maneno haya ni ya kuaminika tena ni kweli."
Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu wa Mungu.
Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kujaribu ili kuthibitisha mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza na kamilifu machoni pake.
Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;
usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.
Nitakutia nguvu na kukusaidia;
nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Mwaka wa upendeleo wa Mwenyezi Mungu
Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi yu juu yangu,
kwa sababu Mwenyezi Mungu amenipaka mafuta
kuwahubiria maskini habari njema.
Amenituma kuwafariji waliovunjika moyo,
kuwatangazia mateka uhuru wao,
na hao waliofungwa
habari za kufunguliwa kwao;
kutangaza mwaka wa Mwenyezi Mungu uliokubaliwa,
na siku ya kisasi ya Mungu wetu,
kuwafariji wote wanaoomboleza,
na kuwapa mahitaji
wale wanaohuzunika katika Sayuni,
ili kuwapa taji za uzuri badala ya majivu,
mafuta ya furaha badala ya maombolezo,
vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa.
Nao wataitwa mialoni ya haki,
pando la Mwenyezi Mungu,
ili kuonesha utukufu wake.
Kama mama anavyomfariji mtoto wake,
ndivyo nitakavyokufariji wewe,
nawe utafarijiwa huko Yerusalemu."
Nunca sozinhos
Deus nunca nos abandona. Ele está ao nosso lado em cada vale, segura nossa mão e promete que o choro não durará para sempre.
Mwenyezi Mungu mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike."
Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema,
"Kamwe sitakuacha,
wala sitakupungukia."
Mwenyezi Mungu ni Mwema,
kimbilio wakati wa taabu.
Huwatunza wale wanaomtegemea,
Mwenyezi Mungu, Mungu wako, yu pamoja nawe,
yeye ni Shujaa mwenye nguvu anayeokoa.
Atakufurahia kwa furaha kubwa,
atakutuliza kwa pendo lake,
atakufurahia kwa kuimba."
Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Mwenyezi Mungu, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.
Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Al-Masihi, amekuwa kiumbe kipya: ya kale yamepita; tazama, yamekuwa mapya.
Kwa hiyo, wale wanaoteswa kulingana na mapenzi ya Mungu, wajikabidhi kwa Muumba wao aliye mwaminifu, huku wakizidi kutenda mema.
Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake. Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye anajishughulisha sana na mambo yenu.
Hata nikipita katikati
ya bonde la uvuli wa mauti,
sitaogopa mabaya,
kwa maana wewe upo pamoja nami;
fimbo yako na mkongojo wako
vyanifariji.
Jambo moja ninamwomba Mwenyezi Mungu,
hili ndilo ninalolitafuta:
niweze kukaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu
siku zote za maisha yangu,
niutazame uzuri wa Mwenyezi Mungu
na kumtafuta hekaluni mwake.
Kwa kuwa siku ya shida,
atanihifadhi salama katika maskani yake,
atanificha uvulini mwa hema lake,
na kuniweka juu kwenye mwamba.
Faraja yangu katika mateso yangu ni hii:
Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.
Huwainua juu wanyonge,
nao wale wanaoomboleza
huinuliwa wakawa salama.
Isa akasema, "Amin, nawaambia, hakuna mtu yeyote aliyeacha nyumba, ndugu wa kiume au wa kike, au mama au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu: nyumba, ndugu wa kiume na wa kike, mama na baba na watoto, mashamba pamoja na mateso, kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao.
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi, naye anakaa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima; nitakuja kwenu.