Publicidade

Pensamentos

Por Bíblia Online

A Bíblia ensina que somos fruto dos nossos pensamentos. Por isso, Deus nos chama a renovar a mente, pensar em coisas nobres e guardar o coração com toda diligência.

Pensar no que é bom

Paulo nos exorta a pensar no que é verdadeiro, honesto, justo, puro, amável e de boa fama. A mente renovada é o caminho da transformação.

Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.

Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kujaribu ili kuthibitisha mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza na kamilifu machoni pake.

Mwito wa kuishi maisha matakatifu

Kwa hiyo, tayarisheni nia zenu kwa kazi; mwe na kiasi, mkitumainia kikamilifu ile neema mtakayopewa Isa Al-Masihi atakapodhihirishwa.

Basi kwa yeye awezaye kutenda mambo ya ajabu yasiyopimika kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya uweza wake ule utendao kazi ndani yetu, yeye atukuzwe katika jumuiya ya waumini, na katika Al-Masihi Isa kwa vizazi vyote, milele na milele. Amen.

Guardar a mente

A Palavra de Deus discerne os pensamentos e intenções do coração. Guardar a mente é proteger a alma das armadilhas do pecado.

Kwa maana neno la Mungu li hai tena lina nguvu. Lina makali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili, hivyo linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo,

maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Sawazisha mapito ya miguu yako

na njia zako zote ziwe zimethibitika.

Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,

bali mwisho wake huelekeza mautini.

Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake,

bali Mwenyezi Mungu huupima moyo.

Os caminhos de Deus são mais altos

Os pensamentos de Deus são infinitamente superiores aos nossos. Devemos entregar nossos pensamentos a Ele e confiar em sua sabedoria.

"Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu,

wala njia zenu si njia zangu,"

asema Mwenyezi Mungu.

Mtu mwovu na aiache njia yake,

na mtu mbaya na ayaache mawazo yake.

Yeye na amrudie Mwenyezi Mungu, naye atamrehemu,

arudi kwa Mungu wetu, kwa kuwa atamsamehe bure kabisa.

Mkabidhi Mwenyezi Mungu lolote ufanyalo,

nayo mipango yako itafanikiwa.

Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu,

nijaribu na ujue mawazo yangu.

Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu,

uniongoze katika njia ya milele.

Mwenyezi Mungu asiyeweza kukwepwa

Ee Mwenyezi Mungu, umenichunguza

na kunijua.

Unajua ninapoketi na ninapoinuka;

unatambua mawazo yangu tokea mbali.

Pensamento e conduta

Do coração procedem os males. A Bíblia nos adverte a não se preocupar excessivamente e a ter pensamentos sóbrios e disciplinados.

Akaendelea kusema, "Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi."

Msiwe na wasiwasi

"Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini au mtakunywa nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

Nanyi mnaposali msiseme maneno kama wafanyavyo watu wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasikiwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao.

Maonyo dhidi ya unafiki

Wakati huo, umati mkubwa wa watu maelfu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Isa akaanza kuzungumza kwanza na wanafunzi wake, akawaambia: "Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki wao. Hakuna jambo lolote lililositirika ambalo halitafunuliwa, au lililofichwa ambalo halitajulikana. Kwa hiyo, lolote mlilosema gizani litasikiwa nuruni. Na kile mlichonong’ona masikioni mkiwa kwenye vyumba vya ndani, kitatangazwa juu ya paa.

"Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya lolote zaidi. Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia, mwogopeni huyo! Mnajua kwamba shomoro watano huuzwa kwa senti mbili? Lakini Mungu hamsahau hata mmoja wao. Naam, hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. Hivyo msiogope, kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.

"Ninawaambia kwamba yeyote atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri mbele za malaika wa Mungu. Lakini yeye atakayenikana mimi mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkana mbele ya malaika wa Mungu. Naye kila atakayenena neno baya dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu wa Mungu hatasamehewa.

"Watakapowapeleka katika masinagogi, na mbele ya watawala na wenye mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu namna mtakavyojitetea au mtakavyosema. Kwa maana Roho wa Mungu atawafundisha wakati huo huo mnachopaswa kusema."

Mfano wa tajiri mpumbavu

Mtu mmoja katika umati ule wa watu akamwambia Isa, "Mwalimu, mwambie ndugu yangu tugawane naye urithi wetu."

Lakini Isa akamwambia, "Rafiki, ni nani aliyeniweka mimi kuwa hakimu wenu au msuluhishi juu yenu?" Ndipo Isa akawaambia, "Jihadharini! Jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana maisha ya mtu hayatokani na wingi wa mali alizo nazo."

Kisha akawaambia mfano huu: "Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana. Akawaza moyoni mwake, Nifanye nini? Sina mahali pa kuhifadhi mavuno yangu.

"Ndipo huyo tajiri akasema, Nitafanya hivi: Nitabomoa maghala yangu ya nafaka na kujenga mengine makubwa zaidi na nihifadhi mavuno yangu yote na vitu vyangu. Nami nitaiambia nafsi yangu, "Nafsi, unavyo vitu vingi vizuri ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi. Pumzika; kula, unywe, ufurahi." 

"Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe! Usiku huu uhai wako unatakiwa. Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani?

"Hivyo ndivyo ilivyo kwa wale wanaojiwekea mali lakini hawajitajirishi kwa Mungu."

Msiwe na wasiwasi

Kisha Isa akawaambia wanafunzi wake: "Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. Maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi. Fikirini ndege! Wao hawapandi wala hawavuni, hawana ghala wala popote pa kuhifadhi nafaka; lakini Mungu huwalisha. Ninyi ni wa thamani kuliko ndege! Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake? Kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo, kwa nini basi kuyasumbukia hayo mengine?

"Angalieni maua jinsi yameavyo: Hayafanyi kazi wala hayafumi. Lakini nawaambia, hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya hayo maua. Basi ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya shambani, ambayo leo yapo, na kesho yanatupwa motoni, si atawavika ninyi vizuri zaidi, enyi wa imani haba! Wala msisumbuke mioyoni mwenu mtakula nini au mtakunywa nini. Msiwe na wasiwasi juu ya haya. Watu wa mataifa ya duniani husumbuka sana kuhusu vitu hivi vyote, lakini Baba yenu anafahamu kuwa mnahitaji haya yote. Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na haya yote atawapa pia.

Kuweka hazina mbinguni

"Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa ninyi ufalme. Uzeni mali yenu mkawape maskini. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, mkajiwekee hazina mbinguni isiyokwisha, ambapo mwizi hakaribii wala nondo haharibu. Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo moyo wako utakapokuwa pia.

Kukesha

"Kuweni tayari mkiwa mmevikwa kwa ajili ya huduma na taa zenu zikiwa zinawaka, kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka karamu ya arusi, ili ajapo na kubisha mlango waweze kumfungulia mara moja. Heri wale watumishi ambao bwana wao atakapokuja atawakuta wakiwa wanakesha. Amin, nawaambia, atajifunga mkanda wake na kuwaketisha ili wale, naye atakuja na kuwahudumia. Itakuwa heri kwa watumwa hao ikiwa bwana wao atakapokuja atawakuta wamekesha hata kama atakuja usiku wa manane, au karibu na mapambazuko. Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua saa mwizi atakuja, hangeiacha nyumba yake kuvunjwa. Ninyi nanyi hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia."

Mfano wa mtumishi mwaminifu

Ndipo Petro akamuuliza, "Bwana Isa, mfano huu unatuambia sisi peke yetu au watu wote?"

Isa akamjibu, "Ni yupi basi wakili mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamfanya msimamizi juu ya watumishi wake wote, ili awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa? Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. Amin nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. Lakini kama yule mtumishi atasema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kurudi,kisha akaanza kuwapiga wale watumishi, wa kiume na wa kike, na kula na kunywa na kulewa. Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wale wasioamini.

"Yule mtumishi anayefahamu vyema mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, atapigwa kwa mapigo mengi. Lakini yeyote ambaye hakujua naye akafanya yale yastahiliyo kupigwa, atapigwa kidogo. Yeyote aliyepewa vitu vingi, atadaiwa vingi; na yeyote aliyekabidhiwa vingi, kwake vitatakiwa vingi.

Isa kuleta mafarakano

"Nimekuja kuleta moto duniani; laiti kama ungekuwa tayari umewashwa! Lakini ninao ubatizo ambao lazima nibatizwe, nayo dhiki yangu ni kuu hadi ubatizo huo ukamilike! Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? La, nawaambia sivyo, nimekuja kuleta mafarakano. Kuanzia sasa, kutakuwa na watu watano katika nyumba moja, watatu dhidi ya wawili, na wawili dhidi ya watatu. Watafarakana baba dhidi ya mwanawe na mwana dhidi ya babaye, mama dhidi ya bintiye na binti dhidi ya mamaye, naye mama mkwe dhidi ya mkwewe na mkwe dhidi ya mama mkwe wake."

Kutambua majira

Pia Isa akaambia umati ule wa watu, "Mwonapo wingu likitokea magharibi, mara mwasema, Mvua itanyesha,nayo hunyesha. Nanyi mwonapo upepo wa kusini ukivuma, ninyi husema, Kutakuwa na joto,na huwa hivyo. Enyi wanafiki! Mnajua jinsi ya kutambua kuonekana kwa dunia na anga. Inakuwaje basi kwamba mnashindwa kutambua wakati huu wa sasa?

"Kwa nini hamwamui wenyewe lililo haki? Ukiwa njiani na mshtaki wako kwenda kwa hakimu, jitahidi kupatana naye mkiwa njiani. La sivyo, atakupeleka kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa afisa, naye afisa atakutupa gerezani. Nakuambia, hutatoka humo hadi uwe umelipa senti ya mwisho."

Ayubu anakamilisha maneno yake

"Nimefanya agano na macho yangu

yasimtazame msichana kwa kumtamani.

Kwa ajili ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja miongoni mwenu, asijidhanie kuwa bora kuliko impasavyo, bali afikiri kwa busara kwa kulingana na kipimo cha imani Mungu aliyompa.

Mgawanyiko katika kundi la waumini

Nawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano kati yenu, na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi.

Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho Mtakatifu wa Mungu.

Msijidanganye. Kama mtu yeyote miongoni mwenu akidhani kuwa ana hekima kwa viwango vya dunia hii, inampasa awe mjinga ili apate kuwa na hekima.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-