Publicidade

O poder da oração

Por Bíblia Online

A oração é o canal mais poderoso de comunicação com Deus. Através dela, milagres acontecem, montanhas são movidas e o impossível se torna possível.

Pedidos com fé

Jesus ensinou: pedi e recebereis. Tudo o que pedirmos em seu nome, crendo, Ele fará. A fé transforma a oração em poder.

Omba, tafuta, bisha

"Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango.

Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea."

Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu.

Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. Mkiniomba lolote kwa Jina langu, nitalifanya.

Oração e milagres

A oração dos justos tem grande poder. Pedro orou e Dorcas ressuscitou. Jesus disse que certos demônios só se expulsam com jejum e oração.

Petro akawatoa wote nje ya kile chumba, kisha akapiga magoti akaomba, akaugeukia ule mwili akasema, "Tabitha, inuka." Akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi.

Isa akawajibu, "Pepo aina hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa kuomba [na kufunga]."

Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi inampasa awaite wazee wa kundi la waumini wamwombee na kumpaka mafuta kwa Jina la Bwana Isa. Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana Isa atamwinua, na kama ametenda dhambi, atasamehewa. Kwa hiyo, ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu, tena yanafaa sana.

Ndipo walipomlilia Mwenyezi Mungu katika shida yao,

naye akawatoa kwenye taabu yao.

Akatuliza dhoruba kwa mnong’ono,

mawimbi ya bahari yakatulia.

Walifurahi ilipokuwa shwari,

naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani.

Orar em todo tempo

A Bíblia nos exorta a orar sem cessar, com ações de graças e súplicas, revestidos da armadura espiritual. A oração traz paz sobrenatural.

Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Al-Masihi Isa.

mkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-28_14-13-17-