Pular para o conteúdo
Publicidade

Preservação das escrituras

Por Bíblia Online

A Palavra de Deus permanece para sempre. As Escrituras foram preservadas por Deus ao longo dos milênios para instrução, consolação e guia de todas as gerações.

A Palavra eterna

Céus e terra passarão, mas as palavras de Deus jamais passarão. Sua Palavra é eterna, infalível e imutável — a verdade que sustenta tudo.

Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.

Majani yakauka, ua lanyauka;

Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.

Maana,

Mwili wote ni kama majani,

Na fahari yake yote ni kama ua la majani.

Majani hukauka na ua lake huanguka;

Bali Neno la Bwana hudumu hata milele.

Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.

Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, linalodumu hata milele. Maana,

Mwili wote ni kama majani,

Na fahari yake yote ni kama ua la majani.

Majani hukauka na ua lake huanguka;

Bali Neno la Bwana hudumu hata milele.

Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.

A inspiração divina

Toda Escritura é inspirada por Deus. Homens santos falaram da parte do Senhor, e a Palavra escrita é a expressão fiel da vontade divina.

Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Mungu amenena katika mwanaye

Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kulia wa Ukuu huko juu;

Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.

A Palavra como guia e tesouro

A Palavra de Deus é lâmpada para os pés, espada do Espírito e tesouro para o coração. Guardá-la e meditá-la nos protege do pecado.

Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,

Nisije nikakutenda dhambi.

Utukufu wa Mungu katika viumbe na hukumu

Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu,

Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.

Mchana husemezana na mchana,

Usiku hutolea usiku maarifa.

Hakuna usemi wala maneno,

Sauti yao haisikilikani.

Sauti yao imeenea duniani kote,

Na maneno yao hadi miisho ya ulimwengu.

Katika hizo ameliwekea jua hema,

Nalo hutokeza kama bwana arusi akitoka chumbani mwake,

Lafurahi kama mtu aliye hodari

Kwenda mbio katika njia yake.

Kuchomoza kwake ni katika mwisho wa mbingu,

Na kuzunguka kwake ni hadi miisho ya mbingu,

Wala hakuna kitu

Kisichofikiwa na joto lake.

Sheria ya BWANA ni kamilifu,

Huiburudisha nafsi.

Ushuhuda wa BWANA ni amini,

Humtia hekima mtu asiye nayo.

Maagizo ya BWANA ni ya adili,

Huufurahisha moyo.

Amri ya BWANA ni safi,

Huyatia macho nuru.

Maneno ya BWANA ni maneno safi,

Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi;

Iliyosafishwa mara saba.

Wewe, BWANA, ndiwe utakayetuhifadhi,

Utatulinda na kizazi hiki milele.

Lakini yanenaje? Lile neno liko karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.

Basi imani, hutokana na kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia,

Sauti yao imeenea duniani kote,

Na maneno yao hadi katika miisho ya ulimwengu.

Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini.

Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.

na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.

Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.

Seja o primeiro