Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 12

Ombi la msaada wakati wa dhiki

Kwa mwimbishaji: kwa kufuata Sheminithi. Zaburi ya Daudi.

1 Isa 57:1 Tuokoe, ee BWANA, maana hamna tena amchaye Mungu

Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.

2 Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe,

Wenye midomo ya kujipendekeza;

Husemezana kwa mioyo ya unafiki;

3 BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza,

Na ulimi unenao maneno ya kiburi;

4 Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda;

Midomo yetu ni yetu wenyewe,

Ni nani aliye bwana juu yetu?

5 Kut 3:7,8 Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge,

Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji,

Sasa nitasimama, asema BWANA,

Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.

6 2 Sam 22:31;Zab 18:30;Mit 30:5 Maneno ya BWANA ni maneno safi,

Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi;

Iliyosafishwa mara saba.

7 Wewe, BWANA, ndiwe utakayetuhifadhi,

Utatulinda na kizazi hiki milele.

8 Wasio haki hutembea pande zote,

Huku ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.

Veja também