Pular para o conteúdo
Publicidade

Protecção e segurança

Por Bíblia Online

Deus é nosso protetor e refúgio seguro. Em todas as circunstâncias, a Bíblia nos assegura que o Senhor guarda, sustenta e protege aqueles que nele confiam.

Deus, a nossa fortaleza

O Senhor é refúgio e fortaleza, socorro bem presente na angústia. Quem habita no esconderijo do Altíssimo descansa à sombra do Todo-Poderoso.

Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,

msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,

msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Mwenyezi Mungu mlinzi wetu

Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana,

atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.

Nitasema kumhusu Mwenyezi Mungu, "Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu, ninayemtumaini."

Atakufunika kwa manyoya yake,

chini ya mabawa yake utapata kimbilio,

uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.

Ijapo watu elfu wataangukia kando yako,

kumi elfu mkono wako wa kuume,

lakini haitakukaribia wewe.

Ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako;

naam, Mwenyezi Mungu ambaye ni kimbilio langu;

basi hakuna madhara yatakayokupata wewe,

hakuna maafa yatalikaribia hema lako.

Sala ya kusifu

Mwenyezi Mungu ni nuru yangu na wokovu wangu,

nimwogope nani?

Mwenyezi Mungu ni ngome ya uzima wangu,

nimhofu nani?

Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu;

yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe.

Mwenyezi Mungu ni kimbilio la wanaodhulumiwa,

ni ngome imara wakati wa shida.

O escudo do Senhor

Deus nos rodeia com sua proteção como um escudo. Ele é rocha, baluarte e libertador. Sua fidelidade nos cobre e nos guarda.

Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ni ngao yangu pande zote;

umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.

Sala ya asubuhi ya kuomba msaada

Ee Mwenyezi Mungu, tazama adui zangu walivyo wengi!

Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!

Wengi wanasema juu yangu,

"Mungu hatamwokoa."

Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ni ngao yangu pande zote;

umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.

Ninamlilia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu,

naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.

Ninajilaza na kupata usingizi;

naamka tena, kwa maana Mwenyezi Mungu hunitegemeza.

Sitaogopa makumi elfu ya adui,

wanaojipanga dhidi yangu kila upande.

Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu,

neno la Mwenyezi Mungu halina dosari.

Yeye ni ngao kwa wote

wanaokimbilia kwake.

Hufanya msaada wa wokovu wako kuwa ngao yangu,

nao mkono wako wa kuume hunitegemeza;

msaada wako umeniinua niwe mkuu.

Huyapanua mapito yangu,

ili miguu yangu isiteleze.

Mfalme amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ushindi

Ahimidiwe Mwenyezi Mungu Mwamba wangu,

aifundishaye mikono yangu vita,

na vidole vyangu kupigana.

Yeye ni Mungu wangu wa upendo na ulinzi wangu,

ngome yangu na mwokozi wangu,

ngao yangu, ninayemkimbilia,

ambaye huwatiisha mataifa chini yangu.

kwa Yule awapaye wafalme ushindi,

ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake,

kutokana na upanga hatari.

Lakini wote wanaokimbilia kwako na wafurahi,

waimbe kwa shangwe daima.

Ueneze ulinzi wako juu yao,

ili wale wanaolipenda jina lako

wapate kukushangilia.

Kwa hakika, Ee Mwenyezi Mungu, unawabariki wenye haki,

unawazunguka kwa wema wako kama ngao.

Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu,

nitegee sikio lako na usikie ombi langu.

Uoneshe ajabu ya upendo wako mkuu,

wewe unayeokoa kwa mkono wako wa kuume

wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.

Nilinde kama mboni ya jicho lako,

unifiche chini ya kivuli cha mabawa yako

kutokana na waovu wanaonishambulia,

kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.

Kwa kuwa mfalme anamtumaini Mwenyezi Mungu;

kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.

Mkono wako utawashika adui zako wote,

mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.

Wakati utajitokeza,

utawafanya kama tanuru la moto.

Katika ghadhabu yake Mwenyezi Mungu atawameza,

moto wake utawateketeza.

Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha,

utaniepusha na taabu

na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.

Segurança e provisão

O Senhor supre todas as necessidades dos seus filhos. Quem busca o Reino primeiro não precisa temer — nada faltará aos que temem ao Senhor.

Mwenyezi Mungu mchungaji wetu

Mwenyezi Mungu ndiye mchungaji wangu,

sitapungukiwa na kitu.

Wana simba wenye nguvu

hutindikiwa na kuona njaa,

bali wale wanaomtafuta Mwenyezi Mungu

hawatakosa kitu chochote kilicho chema.

Mtumaini Mwenyezi Mungu na utende yaliyo mema.

Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.

Nilikuwa kijana na sasa ni mzee,

lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa

au watoto wao wakiombaomba chakula.

Naye Mungu wangu atawajaza ninyi na kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Al-Masihi Isa.

Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Lakini utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.

Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla hamjamwomba.

Omba, tafuta, bisha

"Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango.

Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?

Guarda e livramento

O anjo do Senhor acampa ao redor dos que o temem e os livra. Deus promete guardar todas as nossas saídas e entradas para sempre.

Malaika wa Mwenyezi Mungu hufanya kituo

akiwazunguka wale wamchao,

naye huwaokoa.

Mwenyezi Mungu huwakomboa watumishi wake,

yeyote anayemkimbilia yeye

hatahukumiwa kamwe.

Mwenyezi Mungu mlinzi wetu

Nayainua macho yangu natazama milima:

msaada wangu utatoka wapi?

Msaada wangu hutoka kwa Mwenyezi Mungu,

Muumba wa mbingu na dunia.

Hatauacha mguu wako uteleze,

yeye akulindaye hatasinzia,

hakika, yeye alindaye Israeli

hatasinzia wala hatalala usingizi.

Mwenyezi Mungu anakulinda,

Mwenyezi Mungu ni uvuli wako mkono wako wa kuume,

jua halitakudhuru mchana,

wala mwezi wakati wa usiku.

Mwenyezi Mungu atakukinga na madhara yote,

atayalinda maisha yako,

Mwenyezi Mungu atakulinda unapoingia na unapotoka,

tangu sasa na hata milele.

Sala ya matumaini

Ee Mungu, uniweke salama,

kwa maana kwako nimekimbilia.

Sala ya matumaini

Ee Mungu, uniweke salama,

kwa maana kwako nimekimbilia.

Nimemweka Mwenyezi Mungu mbele yangu daima.

Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,

sitatikisika.

Nimemweka Mwenyezi Mungu mbele yangu daima.

Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,

sitatikisika.

Maombi kwa ajili ya ushindi

Mwenyezi Mungu na akujibu unapokuwa katika dhiki,

jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.

Na akutumie msaada kutoka patakatifu

na akupatie msaada kutoka Sayuni.

Uyalinde maisha yangu na uniokoe,

usiniache niaibike,

kwa maana nimekukimbilia wewe.

Uadilifu na uaminifu vinilinde,

kwa sababu tumaini langu ni kwako, Mwenyezi Mungu.

Farasi ni tumaini la bure kwa wokovu,

licha ya nguvu zake nyingi, hawezi kuokoa.

Lakini macho ya Mwenyezi Mungu yako kwa wale wamchao,

kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo,

ili awaokoe na mauti,

na kuwahifadhi wakati wa njaa.

Sisi tunamngojea Mwenyezi Mungu kwa matumaini,

yeye ni msaada wetu na ngao yetu.

Confiança inabalável

Melhor é confiar no Senhor do que confiar no homem. Quem anda em integridade anda seguro, e a torre forte do nome do Senhor protege o justo.

Mwenyezi Mungu yuko pamoja nami, sitaogopa.

Mwanadamu anaweza kunitenda nini?

Ni bora kumkimbilia Mwenyezi Mungu

kuliko kumtumainia mwanadamu.

Jina la Mwenyezi Mungu ni ngome imara,

wenye haki huikimbilia na kuwa salama.

Jina la Mwenyezi Mungu ni ngome imara,

wenye haki huikimbilia na kuwa salama.

Yeye amchaye Mwenyezi Mungu ana ngome salama,

na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.

kwa kuwa Mwenyezi Mungu atakuwa tumaini lako

na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego.

Mtu mwadilifu hutembea salama,

lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.

"Kila neno la Mungu ni kamilifu;

yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia.

"Kila neno la Mungu ni kamilifu;

yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia.

Haki humlinda mtu mwadilifu,

bali uovu humwangusha mwenye dhambi.

Mwenye haki hula hadi akaridhisha moyo wake,

bali tumbo la mwovu hutaabika kwa njaa.

Kwa maana Mwenyezi Mungu hutoa hekima,

na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.

Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu,

yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,

kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki

na kuhifadhi njia ya waaminifu wake.

Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha,

bali mjinga huendelea mbele, naye hupata madhara.

Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita,

bali ushindi huwa kwa Mwenyezi Mungu.

Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo,

maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

A presença protetora

O Senhor prometeu estar conosco e nunca nos desampara. Ele é como sombra à nossa direita e fortaleza em todo o tempo.

Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anaenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi."

Mungu wa milele ni kimbilio lako,

na chini kuna mikono ya milele.

Atamfukuza adui yako mbele yako,

akisema, Mwangamize yeye!

Kuhusu Benyamini akasema:

"Mwache mpendwa wa Mwenyezi Mungu

apumzike salama kwake,

kwa maana humkinga mchana kutwa,

na yule Mwenyezi Mungu ampendaye

hupumzika kati ya mabega yake."

Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako

itakayofanikiwa,

nawe utauthibitisha kuwa mwongo

kila ulimi utakaokushtaki.

Huu ndio urithi wa watumishi wa Mwenyezi Mungu

na hii ndiyo haki yao inayotoka kwangu,"

asema Mwenyezi Mungu.

Utamlinda katika amani kamilifu

yeye ambaye moyo wake ni thabiti

kwa sababu anakutumaini wewe.

Hata wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye,

Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi.

Nimewahuluku, nami nitawabeba,

nitawahudumia ninyi na kuwaokoa.

Kama ndege warukao,

Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni

ataukinga Yerusalemu;

ataukinga na kuuokoa,

atapita juu yake na kuufanya salama."

Jifunzeni kutenda mema, tafuteni haki.

Wateteeni waliodhulumiwa.

Teteeni shauri la yatima,

wateteeni wajane.

Mkikubali na kutii,

mtakula mema ya nchi,

lakini mkikataa na kuasi,

mtaangamizwa kwa upanga."

Kwa kuwa kinywa cha Mwenyezi Mungu kimenena.

Mwenyezi Mungu atawapigania ninyi, nanyi mnatakiwa kutulia tu."

Mwenyezi Mungu ni Mwema,

kimbilio wakati wa taabu.

Huwatunza wale wanaomtegemea,

Promessas de cuidado

Deus garante que nem um fio de cabelo cairá sem sua permissão. Ele deseja que vivamos em paz, confiança e segurança total nele.

Je, shomoro wawili hawauzwi kwa senti moja tu? Lakini hakuna hata mmoja wao atakayeanguka chini pasipo Baba yenu kujua. Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. Hivyo msiogope; kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.

Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea."

Mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu. Lakini hapatakuwa na unywele mmoja wa kichwa chenu utakaoangamia. Kwa kuvumilia mtaokoa roho zenu.

Mfuko, mkoba na upanga

Kisha Isa akawauliza, "Nilipowatuma bila mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu chochote?"

Wakajibu, "La, hatukupungukiwa na kitu chochote."

Upendo wa Mwenyezi Mungu

Tuseme nini basi kuhusu haya? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyume chetu?

Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri,

"Mwenyezi Mungu ni msaada wangu; sitaogopa.

Mwanadamu anaweza kunitenda nini?"

Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia.

Kwa hiyo basi, tusilale kama watu wengine wanavyolala, bali tukeshe na kuwa na kiasi.

Fidelidade e aliança

Deus é fiel à sua aliança. Ele protege cada promessa que faz e guarda os seus como a menina dos seus olhos.

Lakini Bwana Isa ni mwaminifu, naye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutokana na yule mwovu.

lolote tuombalo, twalipokea kutoka kwake, kwa sababu tumezitii amri zake na kutenda yale yanayompendeza.

Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Nasi kama tunajua atusikia, lolote tuombalo, tunajua kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba.

Tunajua ya kuwa yeye aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, bali aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hawezi kumdhuru.

Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa upotevu, ili Maandiko yapate kutimia.

Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu.

Kwa maana ni nani aliye Mungu

zaidi ya Mwenyezi Mungu?

Ni nani aliye Mwamba

isipokuwa Mungu wetu?

Sasa naomba uwe radhi kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili idumu mbele zako milele, kwa maana wewe, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, umesema, na kwa baraka zako nyumba ya mtumishi wako itaendelea kubarikiwa milele."

Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski, nao Waaramu wakawa watumwa wake na kumlipa ushuru. Mwenyezi Mungu akampa Daudi ushindi kote alipoenda.

Nimekuwa pamoja nawe popote ulipoenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani.

" Fuateni amri zangu na mwe waangalifu kutii amri zangu, nanyi mtaishi salama katika nchi.

Ninaweka agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika; kamwe hakutakuwa tena gharika ya kuangamiza dunia."

Hakika Bwana Mungu Mwenyezi hatafanya neno lolote

bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.

Provisão diária

Deus satisfaz os desejos do coração dos seus filhos. Ele abençoa, renova as forças e sustenta dia após dia quem nele confia.

Ee Mwenyezi Mungu, usinizuilie huruma zako,

upendo wako na kweli yako daima vinilinde.

Mtwike Mwenyezi Mungu fadhaa zako,

naye atakutegemeza,

hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.

Lakini mimi nitaziimba nguvu zako,

asubuhi nitaimba kuhusu upendo wako;

kwa maana wewe ndiwe ngome yangu

na kimbilio langu wakati wa shida.

Bali mfalme atafurahi katika Mungu,

wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu,

bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa.

Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake,

mtukuzeni yeye anayepita juu ya mawingu:

jina lake ni Mwenyezi Mungu,

furahini mbele zake.

Baba wa yatima, mtetezi wa wajane,

ni Mungu katika makao yake matakatifu.

Ahimidiwe Bwana, Mungu Mwokozi wetu,

ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu.

Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mungu wako,

niliyekutoa nchi ya Misri.

Panua sana kinywa chako

nami nitakijaza.

Kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu ni jua na ngao;

Mwenyezi Mungu hutoa wema na heshima;

hakuna kitu chema anachowanyima

wale ambao hawana hatia.

Wale wanaompenda Mwenyezi Mungu na wauchukie uovu,

kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake

na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu.

Mwenyezi Mungu huwalinda wanyenyekevu,

nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.

Ee nafsi yangu, tulia tena,

kwa kuwa Mwenyezi Mungu amekuwa mwema kwako.

Kwa kuwa wewe, Ee Mwenyezi Mungu,

umeniokoa nafsi yangu na mauti,

macho yangu kutokana na machozi,

miguu yangu kutokana na kujikwaa,

ili niweze kutembea mbele za Mwenyezi Mungu,

katika nchi ya walio hai.

Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu,

nimeweka tumaini langu katika neno lako.

Bila Mwenyezi Mungu, kazi ya mwanadamu haifai

Mwenyezi Mungu asipoijenga nyumba,

wajengao hufanya kazi bure.

Mwenyezi Mungu asipoulinda mji,

walinzi wakesha bure.

"Hapa nitamchipushia Daudi pembe,

na kuweka taa kwa ajili ya masiya wangu.

Adui zake nitawavika aibu,

bali taji kichwani pake litang’aa sana."

Mwenyezi Mungu atatimiza kusudi lake kwangu,

Ee Mwenyezi Mungu, upendo wako wadumu milele:

usiziache kazi za mikono yako.

Waufumbua mkono wako,

watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.

Naye huwapatia haki waliodhulumiwa,

na kuwapa wenye njaa chakula.

Mwenyezi Mungu huwaweka wafungwa huru,

Mwenyezi Mungu huwafumbua vipofu macho,

Mwenyezi Mungu huwainua waliolemewa na mizigo yao,

Mwenyezi Mungu huwapenda wenye haki.

Mwenyezi Mungu huwalinda wageni

na kuwategemeza yatima na wajane,

lakini hupinga njia za waovu.

Nitajilaza chini na kulala kwa amani,

kwa kuwa wewe peke yako, Ee Mwenyezi Mungu,

waniwezesha kukaa kwa salama.

Vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kuzipinga hila za ibilisi.

Vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kuzipinga hila za ibilisi. Kwa maana kushindana kwetu si dhidi ya mwili na damu, bali dhidi ya falme na mamlaka, dhidi ya wakuu wa ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

"Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia mimi.

"Lakini mnauliza, Tunakuibia kwa namna gani?

"Mnaniibia zaka na dhabihu. Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi. Leteni zaka kamili ghalani, ili kuwe na chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili," asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, "nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi hata mkose nafasi ya kutosha.

Nitawabariki wao pamoja na maeneo yanayozunguka kilima changu. Nitawanyeshea mvua kwa majira yake, kutakuwa na mvua za baraka.

Hekima ni ulinzi

kama fedha ilivyo ulinzi,

lakini faida ya maarifa ni hii:

kwamba hekima huhifadhi maisha ya aliye nayo.

Vivyo hivyo, Bwana Isa ameamuru kwamba wale wanaohubiri Injili wapate riziki yao kutokana na Injili.

Kwa maana kupenda fedha ndiyo shina moja la maovu ya kila namna. Baadhi ya watu wakitamani fedha, wameiacha imani na kujichoma wenyewe kwa maumivu mengi.

Nitawaburudisha waliochoka na kuwatuliza walio na huzuni."

Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile.

Seja o primeiro