Publicidade

Proximidade

Por Bíblia Online

Deus é próximo dos que o buscam. Ele não é um Deus distante, mas presente, íntimo e acessível a todo o que o invoca com sinceridade de coração.

Buscar a presença de Deus

A Bíblia nos exorta a buscar a face do Senhor continuamente. Quem se aproxima dele encontra plenitude de alegria e delícias perpétuas.

Mtafuteni Mwenyezi Mungu na nguvu zake,

utafuteni uso wake siku zote.

Mtafuteni Mwenyezi Mungu na nguvu zake;

utafuteni uso wake siku zote.

Mtafuteni Mwenyezi Mungu maadamu anapatikana;

mwiteni maadamu yu karibu.

Jambo moja ninamwomba Mwenyezi Mungu,

hili ndilo ninalolitafuta:

niweze kukaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu

siku zote za maisha yangu,

niutazame uzuri wa Mwenyezi Mungu

na kumtafuta hekaluni mwake.

Siku moja katika nyua zako ni bora

kuliko siku elfu mahali pengine;

afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu

kuliko kukaa katika mahema ya waovu.

Umenijulisha njia ya uzima;

utanijaza na furaha mbele zako,

pamoja na furaha ya milele

katika mkono wako wa kuume.

Deus está perto

O Senhor está perto dos que o invocam, dos quebrantados de coração e dos que clamam por socorro. Sua presença nos sustenta.

Wenye haki hulia, naye Mwenyezi Mungu huwasikia,

huwaokoa katika taabu zao zote.

Mwenyezi Mungu yu karibu na waliovunjika moyo,

na huwaokoa waliopondeka roho.

Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana Isa yu karibu.

Lakini sasa katika Al-Masihi Isa, ninyi ambao hapo kwanza mlikuwa mbali na Mungu, sasa mmeletwa karibu kupitia kwa damu ya Al-Masihi.

Hakika wema na upendo vitanifuata

siku zote za maisha yangu,

nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu

milele.

A presença que nunca abandona

Deus promete nunca nos deixar. Ele permanece fiel, está conosco em todo tempo e envia o Espírito para habitar em nossos corações.

Sitawaacha ninyi yatima; nitakuja kwenu.

Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, na awe pamoja nasi kama alivyokuwa na baba zetu, kamwe asituache wala kutukataa.

Lakini kwa rehema zako kuu hukuwakomesha wala kuwaacha, kwa kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na rehema.

Salamu za mwisho

Basi, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa kila njia. Mwenyezi Mungu awe nanyi nyote.

Salamu za mwisho

Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, farijianeni, kuweni na nia moja, na mkae kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.

Tunajua kwamba twakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupatia sisi sehemu ya Roho wake Mtakatifu.

Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba, ndiye ambaye amemdhihirisha.

Musa alikuwa huko pamoja na Mwenyezi Mungu kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya agano, yaani zile Amri Kumi.

waponyeni wagonjwa waliomo na waambieni: Ufalme wa Mungu umewakaribia.

Asa afanya matengenezo

Roho wa Mungu akamjia Azaria mwana wa Odedi. Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, "Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini mkimwacha, naye atawaacha. Kwa muda mrefu Israeli walikuwa hawana Mungu wa kweli, walikuwa hawana kuhani wa kuwafundisha na wala hawakuwa na sheria. Lakini katika taabu yao walimrudia Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, na kumtafuta, naye akaonekana kwao. Katika siku hizo hapakuwa na amani kwa yeyote aliyesafiri, kutoka wala kuingia, kwa kuwa wakazi wote wa nchi walikuwa katika machafuko makubwa. Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina. Lakini ninyi, kuweni hodari wala msikate tamaa, kwa kuwa mtapata thawabu kwa kazi yenu."

Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Odedi yule nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka miji aliyoiteka katika nchi ya vilima ya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu.

Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni walioishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwamba Mwenyezi Mungu, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.

Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa. Wakati huo wakamtolea Mwenyezi Mungu dhabihu za ng’ombe mia saba, kondoo na mbuzi elfu saba kutoka nyara walizoteka. Wakafanya agano kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote. Wale wote ambao hawangemtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke. Wakamwapia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu, kwa kelele, na kupiga tarumbeta na mabaragumu. Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akawapa amani pande zote.

Mfalme Asa akamwondolea Maaka, bibi yake, wadhifa wake kama mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo, akaivunjavunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni. Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia katika Israeli, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Mwenyezi Mungu kikamilifu maisha yake yote. Akaleta ndani ya Hekalu la Mungu fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.

Hapakuwa na vita tena hadi mwaka wa thelathini na tano wa utawala wake Asa.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-29_22-07-56-