Pular para o conteúdo
Publicidade

Redentor

Por Bíblia Online

Deus é o nosso Redentor. Ele nos resgatou da escravidão do pecado, nos libertou das cadeias e nos comprou com preço altíssimo — o sangue de seu Filho.

Liberdade em Cristo

Cristo nos libertou para a liberdade. Aquele a quem o Filho liberta é verdadeiramente livre. O Redentor quebra toda cadeia.

Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.

Uhuru ndani ya Al-Masihi

Al-Masihi alitupatia uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na nira ya utumwa.

Mwaka wa upendeleo wa Mwenyezi Mungu

Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi yu juu yangu,

kwa sababu Mwenyezi Mungu amenipaka mafuta

kuwahubiria maskini habari njema.

Amenituma kuwafariji waliovunjika moyo,

kuwatangazia mateka uhuru wao,

na hao waliofungwa

habari za kufunguliwa kwao;

Maisha katika Roho wa Mungu

Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu ya adhabu kwa wale walio ndani ya Al-Masihi Isa. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Al-Masihi Isa imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Redenção e salvação

Deus nos redimiu por amor. Ele apagou nossas transgressões e nos salvou não por mérito nosso, mas por sua misericórdia.

Nimeyafuta makosa yako kama wingu,

dhambi zako kama ukungu wa asubuhi.

Nirudie mimi,

kwa kuwa nimekukomboa wewe."

Naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina Isa kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua; maana yake Yehova ni wokovu., kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao."

Ndiye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe kutoka uovu wote na kujisafishia watu kuwa mali yake Mwenyewe, yaani wale walio na juhudi katika kutenda mema.

Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakatifu, ambao mwisho wake ni uzima wa milele.

Refúgio e proteção

O Redentor é nosso refúgio e fortaleza. Ele livra os que clamam, sara os quebrantados e se alegra por nós com cântico.

Wimbo wa Daudi wa ushindi

Nakupenda wewe, Ee Mwenyezi Mungu,

nguvu yangu.

Mwenyezi Mungu ni mwamba wangu,

ngome yangu na mwokozi wangu;

Mungu wangu ni mwamba wangu,

ninayemkimbilia.

Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu,

ngome yangu.

Maombi na sifa kwa kuokolewa kutoka kwa adui

Ee Mwenyezi Mungu, nimekukimbilia wewe,

usiache nikaaibika kamwe,

kwa haki yako uniokoe.

Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako,

uniokoe mikononi mwa adui zangu

na wale wanifuatiao.

Wenye haki hulia, naye Mwenyezi Mungu huwasikia,

huwaokoa katika taabu zao zote.

Mwenyezi Mungu yu karibu na waliovunjika moyo,

na huwaokoa waliopondeka roho.

Mwenye haki ana mateso mengi,

lakini Mwenyezi Mungu humwokoa nayo yote,

Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie,

kwa ajili ya utukufu wa jina lako;

tuokoe na kutusamehe dhambi zetu

kwa ajili ya jina lako.

Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha

ninapokuimbia sifa,

mimi, ambaye umenikomboa.

Wale wanaompenda Mwenyezi Mungu na wauchukie uovu,

kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake

na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu.

Ee Mwenyezi Mungu, uniokoe kutoka midomo ya uongo

na ndimi za udanganyifu.

Vestidos de salvação

O Redentor nos veste com roupas de salvação e manto de justiça. Ele se alegra por nós e nos cobre com seu amor.

Ninafurahia sana katika Mwenyezi Mungu,

nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu.

Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu,

na kunipamba kwa joho la haki,

kama vile bwana arusi apambavyo

kichwa chake kama kuhani,

na kama bibi arusi ajipambavyo

kwa vito vyake vya thamani.

Mwenyezi Mungu, Mungu wako, yu pamoja nawe,

yeye ni Shujaa mwenye nguvu anayeokoa.

Atakufurahia kwa furaha kubwa,

atakutuliza kwa pendo lake,

atakufurahia kwa kuimba."

Seja o primeiro