Reino
O Reino de Deus é o tema central da pregação de Jesus. Desde o início de seu ministério, Ele proclamou: 'Arrependei-vos, porque é chegado o Reino dos céus.'
O anúncio do Reino
Jesus inaugurou seu ministério proclamando a chegada do Reino. Ele convida todos ao arrependimento e à fé nessa nova realidade.
Tangu wakati huo, Isa alianza kuhubiri akisema: "Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia."
akisema, "Wakati umetimia, ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Injili."
waponyeni wagonjwa waliomo na waambieni: ‘Ufalme wa Mungu umewakaribia.’
Tazama jinsi miguu ya wale waletao habari njema
ilivyo mizuri juu ya milima,
wale wanaotangaza amani,
wanaoleta habari njema,
wanaotangaza wokovu,
wauambiao Sayuni,
"Mungu wako anatawala!"
A natureza do Reino
O Reino de Deus é governo soberano do Senhor sobre todas as coisas. Ele é o Rei eterno, imortal e invisível.
Basi Mfalme wa milele, asiye na mwisho, asiyeonekana, aliye Mungu pekee, apewe heshima na utukufu milele na milele. Amen.
Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Mwenyezi Mungu,
na utukufu na enzi na uzuri,
kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani
ni chako wewe.
Ee Mwenyezi Mungu, ufalme ni wako;
umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.
Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu?
Ni Mwenyezi Mungu,
Mungu wa majeshi ya mbinguni;
yeye ndiye Mfalme wa utukufu.
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwamuzi wetu,
Mwenyezi Mungu ndiye mtoa sheria wetu,
Mwenyezi Mungu ni mfalme wetu,
yeye ndiye atakayetuokoa.
Mwenyezi Mungu atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwa Mwenyezi Mungu mmoja, na jina lake litakuwa jina pekee.
Entrar no Reino
Para entrar no Reino é preciso nascer de novo, tornar-se como criança e buscar primeiro a justiça de Deus acima de tudo.
Isa akamjibu, "Amin, amin nakuambia, hakuna mtu anayeweza kuuona ufalme wa Mungu kama hajazaliwa mara ya pili."
Isa akamwambia, "Amin, amin nakuambia, hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia ufalme wa Mungu kama hajazaliwa kwa maji na kwa Roho.
Lakini utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.
Isa akasema, "Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa wale walio kama hawa."
Heri wanaoteswa kwa sababu ya haki,
maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, nalo lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni."
Cidadãos do Reino
Os cristãos são concidadãos dos santos e membros da família de Deus, chamados a viver dignamente do Reino que receberam.
Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena na wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na watakatifu na pia jamaa wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Al-Masihi Isa ndiye jiwe kuu la pembeni.
Kuweka hazina mbinguni
"Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa ninyi ufalme.
Waliobarikiwa na walio watakatifu ni wale walio na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Hao mauti ya pili haina nguvu juu yao, bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Al-Masihi, nao watatawala pamoja naye kwa muda wa miaka elfu.
Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, wala walawiti, wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyang’anyi hawataurithi ufalme wa Mungu.