Repouso e férias
Deus criou o descanso como parte da vida. O sábado, o repouso e até as férias refletem a confiança de que Deus sustenta todas as coisas — mesmo quando paramos.
O descanso como ordenança
Deus descansou no sétimo dia e nos convidou a fazer o mesmo. O descanso sabático é um presente de Deus para restauração do corpo e da alma.
Basi, limesalia pumziko la sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika pumziko lake amepumzika mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyopumzika katika kazi zake.
Kama ukigeuza mguu wako usiivunje sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo.
Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
Sono e paz
Ditar-se em paz e dormir tranquilamente é bênção do Senhor. Quem confia nele dorme sem medo e acorda renovado.
Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara,
Maana Wewe, BWANA, peke yako,
Ndiwe unijaliaye kukaa salama.
Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena,
Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.
Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema,
Na kukawia kwenda kulala,
Na kula chakula cha taabu;
Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
Hutaogopa hatari za usiku,
Wala mshale urukao mchana,
Ulalapo hutaona hofu;
Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.
Usingizi wake kibarua ni mtamu, awe amekula kidogo, au awe amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi.
Descanso e segurança
No repouso, encontramos segurança. Deus guarda os justos, e mesmo no silêncio da noite, sua paz nos protege e restaura.
Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini;
Naam, utatafutatafuta kando yako, na kupumzika salama.
Tena utalala, wala hapana atakayekutia hofu;
Naam, wengi watakutafuta uso wako.
Yeye huingia katika amani; wao hustarehe katika vitanda vyao, kila mtu aendaye katika unyofu wake.