Pular para o conteúdo
Publicidade

Salvador

Por Bíblia Online

Jesus é o Salvador do mundo. Desde a manjedoura até a cruz e a ressurreição, toda a Escritura aponta para Aquele que veio buscar e salvar o que se havia perdido.

O Salvador nasceu

Na plenitude dos tempos, Deus enviou seu Filho ao mundo. O anjo declarou: 'Hoje vos nasceu um Salvador, que é Cristo, o Senhor.'

Leo katika mji wa Daudi kwa ajili yenu amezaliwa Mwokozi, ndiye Al-Masihi, Bwana.

Yeye, ingawa alikuwa na asili ya Mungu hasa,

hakuona kule kuwa sawa na Mungu

kuwa kitu cha kushikilia,

bali alijifanya si kitu,

akachukua hali hasa ya mtumwa,

naye akazaliwa katika umbo la mwanadamu.

Naye akiwa na umbo la mwanadamu,

alijinyenyekeza, akatii hata mauti:

naam, mauti ya msalaba!

"Bali mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu,

niliyewaleta ninyi toka Misri.

Msimkubali Mungu mwingine ila mimi,

hakuna Mwokozi isipokuwa mimi.

O sacrifício redentor

Jesus deu a própria vida por nós. Ele é a propiciação pelos nossos pecados e o autor da salvação eterna para todos os que lhe obedecem.

Yeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.

Hili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu.

Kwa kuwa kama tulipokuwa adui wa Mungu tulipatanishwa naye kupitia kwa kifo cha Mwanawe, si zaidi sana baada ya kupatanishwa, tutaokolewa kwa uzima wake.

Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka mwenendo wenu usiofaa, ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu. Hamkukombolewa kwa vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu, bali mlikombolewa kwa damu ya thamani ya Al-Masihi, yule Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa.

Ndani yake tunao ukombozi kupitia kwa damu yake, yaani msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake

Nimesulubiwa pamoja na Al-Masihi, wala si mimi tena ninayeishi, bali Al-Masihi ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani katika Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili., aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.

O caminho da salvação

Jesus é o mediador da nova aliança. Ele vive para interceder por nós e pode salvar perfeitamente todos os que se achegam a Deus por meio dele.

naye akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii.

Kwa hiyo anaweza kuwaokoa kabisa wale wanaomjia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye adumu daima kuomba kwa ajili yao.

Kwa sababu hii Al-Masihi ni mpatanishi wa agano jipya, ili wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza.

Basi na tumtazame sana Isa mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kupitia kwa ukombozi ulio katika Al-Masihi Isa.

Hadi leo nimepata msaada kutoka kwa Mungu, na hivyo nasimama hapa nikishuhudia kwa wakubwa na wadogo. Sisemi chochote zaidi ya yale ambayo manabii na Musa walisema yatatukia: kwamba Al-Masihi atateswa, na kwamba yeye atakuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, na atatangaza nuru kwa watu wake na kwa watu wa Mataifa."

Yule malaika akawaambia wale wanawake, "Msiogope, kwa maana ninajua kuwa mnamtafuta Isa aliyesulubiwa. Hayupo hapa, kwa kuwa amefufuka, kama alivyosema. Njooni mpatazame mahali alipokuwa amelazwa.

Ninajua kwamba Mkombozi wangu yu hai,

naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi.

Seja o primeiro