Sonhos
Sonhos aparecem em toda a Bíblia como meio de revelação divina. Deus falou através de sonhos a patriarcas, profetas e servos, mas também alertou contra falsos sonhadores.
Sonhos como revelação divina
Deus usou sonhos para comunicar sua vontade a homens e mulheres ao longo da história bíblica, revelando caminhos e mistérios.
Mwenyezi Mungu akawaambia, "Sikilizeni maneno yangu:
"Akiwepo nabii wa Mwenyezi Mungu miongoni mwenu,
nitajifunua kwake kwa maono,
nitanena naye katika ndoto.
"Hata itakuwa, baada ya hayo,
nitamimina Roho wangu Mtakatifu juu ya wote wenye mwili.
Wana wenu wa kiume na wa kike watatabiri,
wazee wenu wataota ndoto,
na vijana wenu wataona maono.
Ndipo Petro akasimama pamoja na wale mitume kumi na mmoja, akapaza sauti yake na kuhutubia umati ule wa watu, akasema: "Wayahudi wenzangu na nyote mnaoishi Yerusalemu, nisikilizeni kwa makini, ili jambo hili lijulikane kwenu. Hakika watu hawa hawajalewa kama mnavyodhania, kwa kuwa sasa ni saa tatu asubuhi! La, hili ni jambo lililotabiriwa na nabii Yoeli, akisema:
" ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu,
nitamimina Roho wangu
juu ya wote wenye mwili.
Wana wenu wa kiume na wa kike watatabiri,
vijana wenu wataona maono,
na wazee wenu wataota ndoto.
Mungu akawapa hawa vijana wanne maarifa na ufahamu wa kila aina ya maandiko na elimu. Naye Danieli aliweza kufahamu maono na aina zote za ndoto.
Mfalme akamuuliza Danieli (aliyeitwa pia Belteshaza), "Je, unaweza kuniambia nilichoona katika ndoto yangu na kuifasiri?"
Danieli akajibu, "Hakuna mwenye hekima, msihiri, mganga au mwaguzi anayeweza kumweleza mfalme siri aliyouliza, lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri. Amemwonesha Mfalme Nebukadneza kitakachotokea siku zijazo. Ndoto yako na maono yaliyopita mawazoni mwako ulipokuwa umelala kitandani mwako ni haya:
Sonhos na história da Bíblia
De José no Egito a José pai de Jesus, Deus guiou a história da salvação através de sonhos, protegendo e dirigindo seu povo.
Wakamjibu, "Sisi sote tumeota ndoto, lakini hakuna wa kuzifasiri."
Ndipo Yusufu akawaambia, "Je, kufasiri ndoto si ni kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu."
Farao akamwambia Yusufu, "Nimeota ndoto, wala hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuifasiri. Lakini nimesikia habari yako kwamba unapoelezwa ndoto unaweza kuifasiri."
Yusufu akamjibu Farao, "Siwezi kuifasiri, lakini Mungu atampa Farao jibu analolihitaji."
Lakini alipokuwa akifikiri kufanya jambo hili, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea katika ndoto na kusema, "Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho wa Mungu. Naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina Isa kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua; maana yake Yehova ni wokovu., kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao."
Pilato akiwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mkewe akampelekea ujumbe huu: "Usiwe na jambo lolote juu ya mtu huyu asiye na hatia, kwa kuwa leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake."
Mwenyezi Mungu alipowarejesha mateka Sayuni,
tulikuwa kama watu walioota ndoto.
Sabedoria sobre sonhos
A Bíblia ensina discernimento: nem todo sonho vem de Deus. Devemos entregar nossos planos ao Senhor e confiar na direção dele.
Mkabidhi Mwenyezi Mungu lolote ufanyalo,
nayo mipango yako itafanikiwa.
Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu,
lakini kusudi la Mwenyezi Mungu ndilo litakalosimama.
Kama nabii, au yule anayetabiri kupitia ndoto, akijitokeza miongoni mwenu na akawatangazia ishara ya miujiza na ajabu, ikiwa ishara au ajabu ya aliyozungumza ikatokea, naye akasema, "Na tufuate miungu mingine" (miungu ambayo hamjaifahamu) "na tuiabudu," kamwe msiyasikilize maneno ya nabii wala mwota ndoto huyo. Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawajaribu kuangalia kama mnampenda kwa moyo wote na kwa roho yote. Ni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.
"Nimesikia wanayoyasema manabii, hao wanaotabiri uongo kwa jina langu. Wanasema, ‘Nimeota ndoto! Nimeota ndoto!’ Mambo haya yataendelea hata lini ndani ya mioyo ya hawa manabii wa uongo, ambao hutabiri maono ya uongo ya akili zao wenyewe?
Kweli, niko kinyume na hao wanaotabiri ndoto za uongo," asema Mwenyezi Mungu. "Wanazisimulia na kuwapotosha watu wangu kwa uongo wao bila kujali, lakini sikuwatuma wala sikuwaamuru. Hawawafaidi watu hawa hata kidogo," asema Mwenyezi Mungu.
Kama vile ndoto huja
wakati kuna shughuli nyingi,
ndivyo yalivyo mazungumzo ya mpumbavu
wakati kuna maneno mengi.
Kuota ndoto kwingi na maneno mengi ni ubatili. Kwa hiyo mche Mungu.