Temor do Senhor
O temor do Senhor é o princípio da sabedoria. Não se trata de medo, mas de reverência profunda, respeito e admiração diante da santidade e grandeza de Deus.
O princípio da sabedoria
A Escritura afirma que temer ao Senhor é o primeiro passo para a verdadeira sabedoria. Quem teme a Deus discerne o certo e aprende a viver com prudência.
Kumcha Mwenyezi Mungu ndicho chanzo cha hekima,
wote wanaozifuata amri zake wana busara.
Sifa zake zadumu milele.
"Kumcha Mwenyezi Mungu ndicho chanzo cha hekima,
na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
Kumcha Mwenyezi Mungu humfundisha mtu hekima,
nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.
Naye Mungu akamwambia mwanadamu,
"Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,
nako kujitenga na uovu ndio ufahamu."
Kumcha Mwenyezi Mungu ni utakatifu,
nako kwadumu milele.
Amri za Mwenyezi Mungu ni za hakika,
nazo zina haki.
Ni za thamani kuliko dhahabu,
kuliko dhahabu iliyo safi sana,
ni tamu kuliko asali,
kuliko asali kutoka sega.
Kwa hizo mtumishi wako anaonywa,
katika kuzishika kuna thawabu kubwa.
Bênçãos do temor
Quem teme ao Senhor encontra vida longa, provisão e proteção. O temor de Deus nos guarda do mal e nos conduz à humildade.
Unyenyekevu na kumcha Mwenyezi Mungu
huleta utajiri, heshima na uzima.
Kumcha Mwenyezi Mungu huongeza urefu wa maisha,
lakini miaka ya mwovu inafupishwa.
Kumcha Mwenyezi Mungu ni chemchemi ya uzima,
ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.
Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa;
kwa kumcha Mwenyezi Mungu mtu hujiepusha na ubaya.
Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Mwenyezi Mungu,
bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu
huanguka kwenye taabu.
Onjeni mwone kwamba Mwenyezi Mungu ni mwema;
heri mtu yule anayemkimbilia.
Mcheni Mwenyezi Mungu enyi watakatifu wake,
kwa maana wale wamchao
hawapungukiwi na chochote.
Vivendo no temor do Senhor
Temer ao Senhor é obedecer seus mandamentos, andar em seus caminhos e amá-lo de todo coração. Essa reverência se expressa em justiça e integridade.
Ni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.
Shikeni maagizo ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, mtembee katika njia zake na kumheshimu.
Mtumikieni Mwenyezi Mungu kwa hofu
na mshangilie kwa kutetemeka.
Njooni, watoto wangu, mnisikilize,
nitawafundisha kumcha Mwenyezi Mungu.
Yeyote kati yenu anayependa uzima
na kutamani kuziona siku nyingi njema,
basi auzuie ulimi wake na mabaya,
na midomo yake kutokana na kusema uongo.
Aache uovu, atende mema,
aitafute amani na kuifuatilia.
Basi sasa kicho cha Mwenyezi Mungu na kiwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, hakuna jambo la dhuluma, wala upendeleo, wala rushwa."
" ‘Usimlaani kiziwi, wala usiweke kikwazo mbele ya kipofu, lakini umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
Mmoja asimpunje mwingine, bali utamcha Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako.
" ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini, naye akashindwa kujitegemeza mwenyewe kati yako, msaidie vile ungemsaidia mgeni au mkazi wa muda, ili aweze kuendelea kuishi kati yako. Usichukue riba wala faida yoyote kutoka kwake, bali utamwogopa Mungu wako, ili mzawa wa nchi yako aweze kuendelea kuishi kati yako.
"Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya lolote zaidi. Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia, mwogopeni huyo!