Pular para o conteúdo
Publicidade

Sobre ter filhos

Por Bíblia Online

Filhos são uma dádiva do Senhor, uma herança que Deus confia aos pais. A Bíblia celebra a maternidade e a paternidade como vocações sagradas e fontes de bênção.

Filhos: herança do Senhor

A Escritura declara que os filhos são bênção de Deus. Cada criança é um presente precioso confiado aos pais para ser cuidado com amor.

Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA,

Uzao wa tumbo ni thawabu.

Kama mishale mkononi mwa shujaa,

Ndivyo walivyo watoto wa ujanani.

Heri mtu yule

Aliyelijaza podo lake hivyo.

Naam, hawataona aibu

Wanaposema na adui langoni.

Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,

Katika nyumba yako.

Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni

Wakiizunguka meza yako.

Humweka nyumbani mwanamke aliye tasa,

Awe mama ya watoto mwenye furaha.

Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Instruir nos caminhos de Deus

A Bíblia orienta os pais a instruir seus filhos nos caminhos do Senhor desde cedo, com dedicação, disciplina e exemplo.

Mlee mtoto katika njia impasayo,

Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. Nayo wafunzeni watoto wenu kwa kuyazungumza uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

Mrudi mwanao naye atakustarehesha;

Naam, atakufurahisha nafsi yako.

Cada vida é preciosa

Deus conhece e forma cada criança no ventre. Antes de nascer, Ele já nos separou e preparou um propósito para cada vida.

Kabla sijakuumba katika tumbo nilikujua, na kabla hujatoka tumboni, nilikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,

Uliniunga tumboni mwa mama yangu.

Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa

Kwa njia ya ajabu ya kutisha.

Matendo yako ni ya ajabu,

Na nafsi yangu yajua sana,

Mifupa yangu haikusitirika kwako,

Nilipoumbwa kwa siri,

Nilipoungwa kwa ustadi katika pande za chini za nchi;

Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao

Umeiweka misingi ya nguvu;

Kwa sababu yao wanaoshindana nawe;

Uwakomeshe adui na mjilipiza kisasi.

Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.

Seja o primeiro