Mungu msaidizi wa mhitaji
1 Haleluya.
Enyi watumishi wa BWANA, sifuni,
Lisifuni jina la BWANA.
2 Dan 2:20 Jina la BWANA lihimidiwe
Tangu leo na hata milele.
3 Isa 59:19;Hab 2:14;Mal 1:11;Ufu 11:15 Toka maawio ya jua hata machweo yake
Jina la BWANA husifiwa.
4 BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,
Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
5 Ni nani aliye mfano wa BWANA,
Mungu wetu aketiye juu;
6 Isa 57:15 Anyenyekeaye kutazama,
Mbinguni na duniani?
7 1 Sam 2:8;Isa 26:19;Dan 12:2 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
8 Ayu 36:7 Ili amketishe pamoja na wakuu,
Pamoja na wakuu wa watu wake.
9 1 Sam 2:5;Gal 4:27 Humweka nyumbani mwanamke aliye tasa,
Awe mama ya watoto mwenye furaha.