Vida nova
Em Cristo, toda pessoa é transformada em uma nova criação. O velho passa e tudo se faz novo. A vida nova é o resultado da obra redentora de Jesus em nosso coração.
Morte e ressurreição com Cristo
O batismo simboliza nossa morte para o pecado e ressurreição para uma nova vida. Fomos sepultados com Cristo e ressuscitamos com Ele.
Au hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Al-Masihi Isa tulibatizwa katika mauti yake? Kwa hiyo tulizikwa pamoja naye kupitia kwa ubatizo katika mauti, ili kama vile Al-Masihi alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, nasi pia tupate kuishi maisha mapya.
Kwa maana ikiwa tumeungana naye katika mauti yake, bila shaka tutaungana naye katika ufufuo wake. Kwa maana twajua kwamba utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja naye ili ule mwili wa dhambi upate kuangamizwa, nasi tusiendelee kuwa tena watumwa wa dhambi. Kwa maana mtu yeyote aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.
Vivyo hivyo, jihesabuni wafu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Al-Masihi Isa.
Nova criação
Quando aceitamos Jesus, nascemos de novo. A velha natureza dá lugar a uma identidade renovada pelo Espírito Santo.
Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Al-Masihi, amekuwa kiumbe kipya: ya kale yamepita; tazama, yamekuwa mapya.
Nimesulubiwa pamoja na Al-Masihi, wala si mimi tena ninayeishi, bali Al-Masihi ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani katika Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili., aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.
Hapa hakuna Myunani wala Myahudi, aliyetahiriwa wala asiyetahiriwa, asiyestaarabika wala aliyestaarabika, mtumwa wala mtu huru, bali Al-Masihi ni yote, na ndani ya yote.
Despir o velho, vestir o novo
A vida nova se manifesta em abandonar os velhos hábitos e revestir-se do novo homem, criado segundo a vontade de Deus.
Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, ili mfanywe upya katika roho ya nia zenu, na mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki ya kweli na utakatifu.
Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote: yaani hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu. Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake, nanyi mmevaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu sawasawa na mfano wa Muumba wake.
Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutokana na udhalimu wote.
Renovação interior
Deus promete dar um coração novo e um espírito novo. A transformação nasce do arrependimento e da purificação divina.
Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
Usinitupe kutoka mbele zako
wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.
Unirudishie furaha ya wokovu wako,
unipe roho ya utii, ili initegemeze.
Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakasa kutoka uchafu wenu wote na kutoka sanamu zenu zote. Nitawapa moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu, nitaondoa ndani yenu moyo wenu wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama. Nami nitaweka Roho yangu ndani yenu na kuwafanya ninyi mfuate amri zangu na kuwafanya kuwa waangalifu kuzishika sheria zangu.
Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulistahili ghadhabu, kama watu wengine wote. Lakini Mungu kwa upendo wake mwingi kwetu sisi, ambaye ni mwingi wa rehema, hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Al-Masihi Isa, yaani mmeokolewa kwa neema.