7 Basi Sauli akawaambia watumishi wake, "Nitafutieni mwanamke mwaguzi ili nimwendee, nipate kuuliza kwake."
Watumishi wake wakamwambia, "Yuko mwanamke mmoja huko Endori."
15 Samweli akamuuliza Sauli, "Kwa nini unanitaabisha kwa kunipandisha juu?"
Sauli akasema, "Mimi ninasumbuka sana, kwa maana Wafilisti wanapigana vita dhidi yangu, naye Mungu ameniacha. Hanijibu tena wala kwa njia ya manabii wala kwa ndoto. Kwa hiyo nimekuita wewe ili unijulishe la kufanya."