5 Kwa sababu hii hasa, jitahidini sana katika imani yenu kuongeza wema; na katika wema, maarifa; 6 katika maarifa, kiasi; katika kiasi, saburi; katika saburi, utauwa;1:6 Maana yake kumcha Mungu. 7 katika utauwa, upendano wa ndugu; na katika upendano wa ndugu, upendo.
Publicidade