Pular para o conteúdo
Publicidade

Ufunuo 19:11-16

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Aliyepanda Farasi Mweupe

11 Kisha nikaona mbingu imefunguka na hapo mbele yangu akiwepo farasi mweupe, ambaye yeye aliyempanda aliitwa Mwaminifu na Kweli. Yeye huhukumu kwa haki na kufanya vita. 12 Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Ana jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu yeyote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe. 13 Amevaa joho lililochoviwa katika damu, na Jina lake ni "Neno la Mungu." 14 Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani safi, nyeupe na nzuri. 15 Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. "Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma." Hulikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mungu Mwenyezi. 16 Kwenye joho lake na paja lake pameandikwa jina hili:

Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    11 Kisha nikaona mbingu imefunguka na hapo mbele yangu akiwepo farasi mweupe, ambaye yeye aliyempanda aliitwa Mwaminifu na Kweli. Yeye huhukumu kwa haki na kufanya vita. 12 Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Ana jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu yeyote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe. 13 Amevaa joho lililoloweshwa katika damu, na Jina lake ni Neno la Mungu. 14 Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani safi, nyeupe na nzuri. 15 Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. "Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma." Hulikanyaga shinikizo la ghadhabu ya Mungu Mwenyezi. 16 Kwenye joho lake na paja lake pameandikwa jina hili:

    Mfalme wa wafalme

    na Bwana wa mabwana.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    11 Eze 1:1;Zab 96:13;Isa 11:4;Ufu 3:14Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. 12 Dan 10:6;Ufu 1:14;2:18;3:12Na macho yake yalikuwa kama muali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. 13 Isa 63:1;Yn 1:1Naye amevikwa vazi lililoloweshwa katika damu, na jina lake anaitwa, Neno la Mungu. 14 Ufu 17:14Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. 15 Zab 2:9;Isa 11:4;63:3;Yoe 3:13;Ufu 14:20;12:5Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili kwa upanga huo awapige mataifa. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. 16 Kum 10:17;Dan 2:47;Ufu 17:14;1 Tim 6:15Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.