Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 16:9-12

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

9 Wakati wa usiku Paulo akaona maono, mtu wa Makedonia amesimama akimsihi, "Vuka uje huku Makedonia utusaidie." 10 Baada ya Paulo kuona maono haya, tulijiandaa kwa haraka kuondoka kwenda Makedonia tukiwa tumesadiki kuwa Mungu alikuwa ametuita kuhubiri habari njema huko.

Kuokoka Kwa Lidia

11 Tukasafiri kwa njia ya bahari kutoka Troa na kwenda moja kwa moja hadi Samothrake, kesho yake tukafika Neapoli. 12 Kutoka huko tukasafiri hadi Filipi, mji mkuu wa jimbo hilo la Makedonia, uliokuwa koloni ya Warumi. Nasi tukakaa huko siku kadhaa.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    9 Wakati wa usiku Paulo akaona maono, mtu wa Makedonia amesimama akimsihi, "Vuka uje huku Makedonia utusaidie." 10 Baada ya Paulo kuona maono haya, tulijiandaa kwa haraka kuondoka kwenda Makedonia tukiwa tumesadiki kuwa Mungu alikuwa ametuita kuhubiri Injili huko.

    11 Tukasafiri kwa meli kutoka Troa na kwenda moja kwa moja hadi Samothrake, na kesho yake tukafika Neapoli. 12 Kutoka huko tukasafiri hadi Filipi, mji mkuu wa jimbo hilo la Makedonia, uliokuwa koloni ya Warumi. Nasi tukakaa huko siku kadhaa.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    9 Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. 10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubirie Habari Njema.

    11 Basi tukang’oa nanga kutoka Troa, tukafika Samothrake kwa tanga moja, na siku ya pili tukafika Neapoli; 12 na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukakaa siku kadhaa.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.