9 Wakati wa usiku Paulo akaona maono, mtu wa Makedonia amesimama akimsihi, "Vuka uje huku Makedonia utusaidie." 10 Baada ya Paulo kuona maono haya, tulijiandaa kwa haraka kuondoka kwenda Makedonia tukiwa tumesadiki kuwa Mungu alikuwa ametuita kuhubiri Injili huko.
Kuokoka kwa Lidia
11 Tukasafiri kwa meli kutoka Troa na kwenda moja kwa moja hadi Samothrake, na kesho yake tukafika Neapoli. 12 Kutoka huko tukasafiri hadi Filipi, mji mkuu wa jimbo hilo la Makedonia, uliokuwa koloni ya Warumi. Nasi tukakaa huko siku kadhaa.