Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 19:1-3

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Paulo Huko Efeso

1 Apolo alipokuwa huko Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso. Huko akawakuta wanafunzi kadhaa, 2 akawauliza, "Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?"

Wakajibu, "Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu." 3 Ndipo Paulo akawauliza, "Je, mlibatizwa kwa ubatizo gani?" Wakajibu, "Kwa ubatizo wa Yohana."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Apolo alipokuwa huko Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso. Huko akawakuta wanafunzi kadhaa, 2 akawauliza, "Je, mlipokea Roho wa Mungu mlipoamini?"

    Wakajibu, "Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho wa Mungu." 3 Ndipo Paulo akawauliza, "Je, mlibatizwa kwa ubatizo gani?" Wakajibu, "Kwa ubatizo wa Yahya."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadhaa huko; 2 Mdo 2:38akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.