Paulo huko Efeso
1 Apolo alipokuwa huko Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso. Huko akawakuta wanafunzi kadhaa, 2 akawauliza, "Je, mlipokea Roho wa Mungu mlipoamini?"
Wakajibu, "Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho wa Mungu." 3 Ndipo Paulo akawauliza, "Je, mlibatizwa kwa ubatizo gani?" Wakajibu, "Kwa ubatizo wa Yahya."