Pular para o conteúdo
Publicidade

Ezra 2

Orodha Ya Watu Waliorudi Kutoka Uhamishoni

1 Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 2 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):

Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:

3 wazao wa Paroshi 2,172

4 wazao wa Shefatia 372

5 wazao wa Ara 775

6 wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,812

7 wazao wa Elamu 1,254

8 wazao wa Zatu 945

9 wazao wa Zakai 760

10 wazao wa Bani 642

11 wazao wa Bebai 623

12 wazao wa Azgadi 1,222

13 wazao wa Adonikamu 666

14 wazao wa Bigwai 2,056

15 wazao wa Adini 454

16 wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98

17 wazao wa Besai 323

18 wazao wa Yora 112

19 wazao wa Hashumu 223

20 wazao wa Gibari 95

21 watu wa Bethlehemu 123

22 watu wa Netofa 56

23 watu wa Anathothi 128

24 watu wa Azmawethi 42

25 wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743

26 wazao wa Rama na Geba 621

27 watu wa Mikmashi 122

28 watu wa Betheli na Ai 223

29 wazao wa Nebo 52

30 wazao wa Magbishi 156

31 wazao wa Elamu ile ingine 1,254

32 wazao wa Harimu 320

33 wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 725

34 wazao wa Yeriko 345

35 wazao wa Senaa 3,630

36 Makuhani:

wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973

37 wazao wa Imeri 1,052

38 wazao wa Pashuri 1,247

39 wazao wa Harimu 1,017

40 Walawi:

wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia) 74

41 Waimbaji:

wazao wa Asafu 128

42 Mabawabu wa lango la Hekalu:

wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai 139

43 Watumishi wa Hekalu:2:43 Yaani Wanethini (pia 2:58, 70).

wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,

44 wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,

45 wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,

46 wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,

47 wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,

48 wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,

49 wazao wa Uza, Pasea, Besai,

50 wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,

51 wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,

52 wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,

53 wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,

54 wazao wa Nesia na Hatifa.

55 Wazao wa watumishi wa Solomoni:

wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,

56 wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,

57 wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.

58 Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392

59 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:

60 wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 652

61 Kutoka miongoni mwa makuhani:

Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).

62 Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 63 Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.2:63 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.

64 Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 65 tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200. 66 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, 67 ngamia 435 na punda 6,720.

68 Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. 69 Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,0002:69 Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500. za dhahabu, mane 5,0002:69 Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900. za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.

70 Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também