3 Kisha mfalme aliuliza, "Malkia Esta, ni nini? Ombi lako ni nini? Hata kama ni nusu ya ufalme, utapewa."
4 Esta akajibu, "Kama itampendeza mfalme, mfalme pamoja na Hamani waje leo katika karamu ambayo nimeiandaa kwa ajili yake."
8 Kama mfalme ameona vyema, nami nimepata kibali kwake na kama ikimpendeza mfalme kunipa ombi langu na kunitimizia haja yangu, mfalme na Hamani waje kwangu kesho katika karamu nitakayowaandalia. Kisha nitajibu swali la mfalme."
14 Zereshi mkewe na rafiki zake wote wakamwambia, "Tengeneza mahali pa kuangika watu kimo chake dhiraa hamsini,5:14 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5. kisha kesho asubuhi mwombe mfalme Mordekai aangikwe juu yake. Ndipo uende na mfalme kwenye karamu kwa furaha." Shauri hili lilimpendeza Hamani, naye akajenga mahali pa kuangika watu.