Pular para o conteúdo
Publicidade

Esta 5:3,4,8,14

SRUV Swahili Revised Union Version

3 Mk 6:23Mfalme akamwambia, malkia Esta, unataka nini? Nayo ni haja gani uliyo nayo? Utapewa hata nusu ya ufalme. 4 Esta akasema, Mfalme akiona vema, na aje leo, mfalme na Hamani, kwenye karamu niliyomwandalia. 8 Ikiwa nimepata kibali machoni pa mfalme, na mfalme akiona vema kunipa niombalo, na kunitimizia haja yangu, na aje tena mfalme na Hamani kwenye karamu nitakayowaandalia, nami kesho nitafanya kama vile mfalme alivyosema.

14 Est 6:4;7:10;Zab 59:7;Mit 1:16Basi Zereshi mkewe na marafiki wote wa Hamani wakamwambia, Na kitengenezwe kiunzi cha mti wa kunyongea wa urefu wa mikono hamsini, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa furaha pamoja na mfalme karamuni. Basi ushauri huu ukamridhisha Hamani, akautengeneza mti wa kunyongea.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    3 Kisha mfalme aliuliza, "Malkia Esta, ni nini? Ombi lako ni nini? Hata kama ni nusu ya ufalme, utapewa."

    4 Esta akajibu, "Kama itampendeza mfalme, mfalme pamoja na Hamani waje leo katika karamu niliyomwandalia."

    8 Kama mfalme ameona vyema, nami nimepata kibali kwake, na ikimpendeza mfalme kunipa ombi langu na kunitimizia haja yangu, mfalme na Hamani waje kwangu kesho katika karamu nitakayowaandalia. Kisha nitajibu swali la mfalme."

    14 Zereshi mkewe na rafiki zake wote wakamwambia, "Tengeneza mahali pa kuangika watu kimo chake dhiraa hamsini5:14 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5., kisha kesho asubuhi mwombe mfalme Mordekai aangikwe juu yake. Ndipo uende na mfalme kwenye karamu kwa furaha." Shauri hili lilimpendeza Hamani, naye akajenga mahali pa kuangika watu.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    3 Kisha mfalme aliuliza, "Malkia Esta, ni nini? Ombi lako ni nini? Hata kama ni nusu ya ufalme, utapewa."

    4 Esta akajibu, "Kama itampendeza mfalme, mfalme pamoja na Hamani waje leo katika karamu ambayo nimeiandaa kwa ajili yake."

    8 Kama mfalme ameona vyema, nami nimepata kibali kwake na kama ikimpendeza mfalme kunipa ombi langu na kunitimizia haja yangu, mfalme na Hamani waje kwangu kesho katika karamu nitakayowaandalia. Kisha nitajibu swali la mfalme."

    14 Zereshi mkewe na rafiki zake wote wakamwambia, "Tengeneza mahali pa kuangika watu kimo chake dhiraa hamsini,5:14 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5. kisha kesho asubuhi mwombe mfalme Mordekai aangikwe juu yake. Ndipo uende na mfalme kwenye karamu kwa furaha." Shauri hili lilimpendeza Hamani, naye akajenga mahali pa kuangika watu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.