1 Mwa 10:5;Zab 72:10;Isa 24:15 Basi mfalme Ahasuero alitoza kodi katika nchi na katika visiwa vya bahari. 2 Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Umedi na Uajemi? 3 Mwa 41:40;2 Nya 28:7;Neh 2:10;Zab 122:8;Mit 12:20;Isa 26:12 Kwa maana Mordekai Myahudi akiwa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwajali watu wake, na kuiangalia hali njema ya wazawa wao wote.
Publicidade