Pular para o conteúdo
Publicidade

Hosea 12

1 2 Fal 17:4;Isa 30:6 Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.

Uasi wa muda mrefu

2 BWANA naye ana shutuma juu ya Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.

3 Mwa 25:26 Tumboni alimshika ndugu yake kisigino;

Na alipokuwa mtu mzima alishindana na Mungu;Mwa 32:24-26

4 Mwa 28:10-22 Naam, alishindana na malaika

Akashinda; alilia, na kumsihi;

Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;

5 Naam, BWANA, Mungu wa majeshi;

BWANA ndilo kumbukumbu lake.

6 Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.

7 Ni mfanya biashara, aliye na mizani ya udanganyifu mkononi mwake; anapenda kudhulumu. 8 Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wowote uliokuwa dhambi. 9 Law 23:42-43 Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za sikukuu teule. 10 Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano. 11 Amo 4:4 Katika Gileadi kuna uovu? Nao wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng’ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.

12 Mwa 29:1-20 Na Yakobo alikimbia mpaka Padan-Aramu,

Na Israeli alitumika apate mke;

Ili apate mke alichunga kondoo.

13 Kut 12:50-51 Na kwa nabii BWANA alimtoa Israeli katika Misri,

Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.

14 Kum 28:37;Dan 11:18 Efraimu amenitia hasira kali sana; kwa sababu hiyo damu yake itaachwa juu yake, na Bwana wake atamrudishia lawama yake.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também