4 Kisha Bwana akamwambia Mose, "Nitanyesha mikate kutoka mbinguni kwa ajili yenu. Watu watatoka kila siku na kukusanya kitakachowatosha kwa siku ile, kwa njia hii, nitawajaribu nione kama watafuata maelekezo yangu. 5 Siku ya sita watatayarisha kile waletacho ndani, nacho kitakuwa mara mbili kuliko ya kile walichokusanya kila siku."
14 Wakati umande ulipoondoka, vipande vidogo vidogo kama theluji vilionekana juu ya uso wa jangwa. 15 Waisraeli walipoona, wakaambiana, "Hiki ni nini?" Kwa kuwa hawakujua kilikuwa kitu gani.
Mose akawaambia, "Huu ndio mkate ambao Bwana amewapa mle.