4 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, "Tazama! Nitawanyeshea mikate kutoka mbinguni. Watu watatoka kila siku na kukusanya kitakachowatosha kwa siku ile, kwa njia hii, nitawajaribu nione kama watafuata maelekezo yangu. 5 Siku ya sita watatayarisha kile waletacho ndani, nacho kitakuwa mara mbili kuliko ya kile walichokusanya kila siku."
14 Umande ulipoondoka, vipande vidogo vidogo kama theluji vilionekana juu ya mchanga wa jangwa. 15 Waisraeli walipoona, wakaambiana, "Hiki ni nini?" Kwa kuwa hawakujua kilikuwa kitu gani.
Musa akawaambia, "Huu ndio mkate ambao Mwenyezi Mungu amewapa mle.