10 "Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu,25:10 Dhiraa mbili na nusu ni sawa na sentimita 112.5. upana wa dhiraa moja na nusu,25:10 Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5. na kimo cha dhiraa moja na nusu. 11 Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. 12 Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 13 Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 14 Utaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. 15 Hiyo mipiko itabakia daima katika hizo pete za hilo Sanduku; haitaondolewa.
Kutoka 25:10-15
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
10 "Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu25:10 Dhiraa mbili na nusu ni sawa na sentimita 112.5., upana wa dhiraa moja na nusu25:10 Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5., na kimo cha dhiraa moja na nusu. 11 Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. 12 Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 13 Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 14 Utaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. 15 Hiyo mipiko itabakia daima katika hizo pete za hilo Sanduku; haitaondolewa.
- SRUV Swahili Revised Union Version
10 Kut 37:1;Kum 10:3;Ebr 9:4Nao na wafanye sanduku la mti wa mjohoro; urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa25:10 Ni urefu wa kutoka kiwiko cha mkono hadi ncha ya kidole kirefu. moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu. 11 Nawe ulifunike kwa dhahabu safi, ulifunike ndani na nje, nawe tia na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote. 12 Nawe subu vikuku vinne vya dhahabu kwa ajili yake, na kuvitia katika miguu yake minne; vikuku viwili upande mmoja, na vikuku viwili upande wake wa pili. 13 Nawe fanya miti mirefu ya mshita na kuifunika dhahabu. 14 Nawe tia hiyo miti katika vile vikuku vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku. 15 1 Fal 8:8Hiyo miti itakaa katika vile vikuku vya sanduku; haitaondolewa.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.