Sanduku la Agano
10 Kut 37:1;Kum 10:3;Ebr 9:4Nao na wafanye sanduku la mti wa mjohoro; urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa25:10 Ni urefu wa kutoka kiwiko cha mkono hadi ncha ya kidole kirefu. moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu. 11 Nawe ulifunike kwa dhahabu safi, ulifunike ndani na nje, nawe tia na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote. 12 Nawe subu vikuku vinne vya dhahabu kwa ajili yake, na kuvitia katika miguu yake minne; vikuku viwili upande mmoja, na vikuku viwili upande wake wa pili. 13 Nawe fanya miti mirefu ya mshita na kuifunika dhahabu. 14 Nawe tia hiyo miti katika vile vikuku vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku. 15 1 Fal 8:8Hiyo miti itakaa katika vile vikuku vya sanduku; haitaondolewa.