Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 31

Bezaleli na Oholiabu

1 BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2 Kut 35:30;1 Nya 2:20 Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda; 3 Kut 35:31;1 Fal 7:14;Isa 28:26;1 Kor 12:4-8 nami nimemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, 4 ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, 5 na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote. 6 Kut 35:34;28:3;36:1 Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kutengeneza vyote nilivyokuagiza; 7 Kut 36:8 yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema; 8 na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote, na madhabahu ya kufukizia uvumba; 9 na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na kitako chake; 10 na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika kwa ajili ya huduma yao ya ukuhani; 11 na mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.

Sheria za Sabato

12 BWANA akasema na Musa, na kumwambia, 13 Law 19:3;26:2;Eze 20:12;44:24 Kisha, nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati yenu na mimi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi. 14 Neh 9:14;Kum 5:12;Isa 56:6;58:13;Eze 20:12;Kut 35:2;Hes 15:35 Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hana budi atauawa; na kila mtu afanyaye kazi siku hiyo, ataondolewa toka kwa watu wake. 15 Mwa 2:2;Kut 16:23;20:8-11;23:12;28:36;34:21;35:2;Law 23:3;Kum 5:12-14 Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa BWANA; kila mtu atakayefanya kazi yoyote katika siku ya Sabato, hana budi atauawa. 16 Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. 17 Kut 20:11;Eze 20:12;Mwa 1:31 Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, akapumzika kwa siku ya saba na kustarehe.

Mbao mbili za mawe ni ushuhuda wa Agano

18 Kut 24:12;32:15;34:28,29;Kum 4:13;5:22;9:10,11;2 Kor 3:3 Hapo BWANA31:18 Katika Kiebrania hakuna neno BWANA ila hutaja nafsi ya tatu umoja jaani: ‘alipokuwa’. alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa kidole cha Mungu.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também