Pular para o conteúdo
Publicidade

Ezekieli 34:2-6

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

2 "Mwanadamu, tabiri juu ya wachungaji wa Israeli, tabiri na uwaambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ole wa wachungaji wa Israeli ambao hujitunza wenyewe tu! Je, haiwapasi wachungaji kutunza kundi la kondoo? 3 Mnakula mafuta ya wanyama, mnavaa mavazi ya sufu na kuchinja kondoo walionona, lakini hamlitunzi kundi. 4 Hamkuwatia nguvu walio dhaifu wala hamkuwaganga wenye maradhi wala kuwafunga waliojeruhiwa. Hamkuwarudisha waliotangatanga wala kuwatafuta wale waliopotea. Badala yake mmewatawala kwa ukali na kwa ukatili. 5 Hivyo walitawanyika kwa sababu hapakuwepo mchungaji, nao walipotawanyika, wakawa chakula cha wanyama wa mwitu wote. 6 Kondoo wangu walitawanyika, wakatangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wa dunia yote bila kuwa na yeyote wa kuwaulizia wala wa kuwatafuta.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    2 "Mwanadamu, tabiri dhidi ya wachungaji wa Israeli, tabiri na uwaambie: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ole kwa wachungaji wa Israeli ambao hujitunza wenyewe tu! Je, haiwapasi wachungaji kutunza kundi la kondoo? 3 Mnakula mafuta ya wanyama, mnavaa mavazi ya sufu na kuchinja kondoo walionona, lakini hamlitunzi kundi. 4 Hamkuwatia nguvu walio dhaifu, wala kuwaganga wenye maradhi, wala kuwafunga waliojeruhiwa. Hamkuwarudisha waliotangatanga wala kuwatafuta wale waliopotea. Badala yake mmewatawala kwa ukali na kwa ukatili. 5 Hivyo walitawanyika kwa sababu hapakuwa na mchungaji, nao walipotawanyika, wakawa chakula cha wanyama mwitu wote. 6 Kondoo wangu walitangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika duniani kote, bila yeyote wa kuwaulizia wala kuwatafuta.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    2 Eze 33:24;Yer 23:1Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo? 3 Isa 56:11;Mik 3:3Mnawala walionona, mnajivika manyoya, mnawachinja walionona; lakini hamwalishi kondoo. 4 Zek 11:16;2 Tim 2:24;Lk 15:4;1 Pet 5:3;Mt 9:36;Isa 56:9Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala. 5 Hes 27:17;1 Fal 22:17;Mt 9:36;Mk 6:34Nao wakatawanyika, kwa sababu hapakuwa na mchungaji; wakawa chakula cha wanyamamwitu, wakatawanyika. 6 Kondoo wangu walitangatanga katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala kuwatafuta.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.