Pular para o conteúdo
Publicidade

Wagalatia 3:26-28

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Watoto Wa Mungu

26 Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika Kristo Yesu kwa njia ya imani. 27 Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Kristo, mmemvaa Kristo. 28 Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    26 Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika Al-Masihi Isa kupitia kwa imani. 27 Kwa maana wote mliobatizwa3:27 Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali. Wafuasi wa Isa Al-Masihi pia wanapokea Roho wa Mungu kama dhibitisho ya imani yao. ndani ya Al-Masihi, mmemvaa Al-Masihi. 28 Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Al-Masihi Isa.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    26 Yn 1:12;Rum 8:17Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. 27 Rum 6:3;13:14Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28 Rum 10:12;1 Kor 12:13Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.