Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 1:20-24

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

20 Mungu akasema, "Kuwepo na viumbe hai tele kwenye maji, nao ndege waruke juu ya dunia katika nafasi ya anga." 21 Kwa hiyo Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mungu akaona kuwa hili ni jema. 22 Mungu akavibariki, akasema, "Zaeni mwongezeke, mkayajaze maji ya bahari, nao ndege waongezeke katika dunia." 23 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tano.

24 Mungu akasema, "Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake." Ikawa hivyo.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    20 Mungu akasema, "Kuwepo na viumbe hai tele kwenye maji, nao ndege waruke juu ya dunia katika nafasi ya anga." 21 Kwa hiyo Mungu akaumba wanyama wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mungu akaona kuwa hili ni jema. 22 Mungu akavibariki, akasema, "Zaeni mwongezeke, mkayajaze maji ya bahari, nao ndege waongezeke katika dunia." 23 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tano.

    24 Mungu akasema, "Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: mifugo, viumbe vinavyotambaa ardhini na wanyama pori, kila kiumbe kulingana na aina yake." Ikawa hivyo.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    20 Zab 104:24Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na viumbe vyenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. 21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 22 Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi. 23 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.

    24 Zab 104:18-23Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.