Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 20:2,5,11-13

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

2 huko Abrahamu akasema kuhusu Sara mkewe, "Huyu ni dada yangu." Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma Sara aletwe, naye akamchukua.

5 Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu,’ naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri njema na mikono safi."

11 Abrahamu akajibu, "Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’ 12 Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti wa baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu. 13 Wakati Bwana aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonyesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapokwenda, kuhusu mimi sema, "Huyu ni kaka yangu." ’ "

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    2 Huko Ibrahimu akasema kuhusu Sara mkewe, "Huyu ni dada yangu." Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akaagiza Sara aletwe, naye akamchukua awe mkewe.

    5 Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu’; naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri safi na mikono safi."

    11 Ibrahimu akajibu, "Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’ 12 Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti ya baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu. 13 Mungu aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapoenda, sema hivi kunihusu, "Huyu ni kaka yangu." ’ "

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    2 Mwa 12:11-15;26:7Abrahamu akanena juu ya Sara mkewe, "Huyu ni dada yangu". Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wakamtwaa Sara. 5 Je! Hukuniambia mwenyewe, "Huyu ni dada yangu?" Na mwanamke mwenyewe naye akasema, "Huyu ni kaka yangu". Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kutojua kwangu, nimefanya hivi. 11 Mwa 42:18;Neh 5:15;Mit 16:6Abrahamu akasema, Kwa kuwa niliona, hakika hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu. 12 Mwa 11:29Hata hivyo, kwa kweli yeye ni dada yangu, yaani binti wa baba yangu na wala sio binti wa mama yangu; ndipo akawa mke wangu. 13 Mwa 12:1,9,10,13Ikawa hapo Mungu aliponisafirisha kutoka nyumba ya baba yangu, nikamwambia, Hii ndiyo fadhili yako, utakayonifanyia. Kila mahali tuingiapo, useme, Huyu ni kaka yangu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.