2 Huko Ibrahimu akasema kuhusu Sara mkewe, "Huyu ni dada yangu." Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akaagiza Sara aletwe, naye akamchukua awe mkewe.
5 Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu’; naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri safi na mikono safi."
11 Ibrahimu akajibu, "Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’ 12 Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti ya baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu. 13 Mungu aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapoenda, sema hivi kunihusu, "Huyu ni kaka yangu." ’ "