2 Kisha Mungu akamwambia, "Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia."
7 Isaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, "Baba yangu!"
Abrahamu akaitika, "Mimi hapa, mwanangu."
Isaki akasema, "Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?"
8 Abrahamu akajibu, "Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa." Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.
13 Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14 Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire.22:14 Yehova-Yire maana yake Bwana atatupa. Mpaka siku ya leo inasemekana, "Katika mlima wa Bwana itapatikana."