Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 22:2,7,8,13,14

SRUV Swahili Revised Union Version

2 2 Nya 3:1;Yn 3:16Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia. 7 Isaka akasema na Abrahamu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? 8 1 Pet 1:19Abrahamu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja. 13 1 Kor 5:7,8Abrahamu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo dume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Abrahamu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14 Abrahamu akapaita mahali hapo Yehova-yire,22:14 Yehova-yire: maana yake ni BWANA atapata. kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.22:14 ‘atatoa’.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    2 Kisha Mungu akamwambia, "Mchukue mwanao, mwana wako wa pekee umpendaye, Isaka, uende nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima nitakaokuambia."

    7 Isaka akamwambia Ibrahimu baba yake, "Baba yangu!"

    Ibrahimu akaitika, "Mimi hapa, mwanangu."

    Isaka akasema, "Moto na kuni zipo. Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?"

    8 Ibrahimu akajibu, "Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa." Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.

    13 Ibrahimu akainua macho, akaona nyuma yake kondoo dume akiwa amenaswa pembe zake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14 Ibrahimu akapaita mahali pale Yehova-Yire.22:14 maana yake Mwenyezi Mungu atapata Hadi leo inasemekana, "Katika mlima wa Mwenyezi Mungu itapatikana."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    2 Kisha Mungu akamwambia, "Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia."

    7 Isaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, "Baba yangu!"

    Abrahamu akaitika, "Mimi hapa, mwanangu."

    Isaki akasema, "Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?"

    8 Abrahamu akajibu, "Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa." Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.

    13 Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14 Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire.22:14 Yehova-Yire maana yake Bwana atatupa. Mpaka siku ya leo inasemekana, "Katika mlima wa Bwana itapatikana."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.