6 Abrahamu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaki mwanawe, yeye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja, 7 Isaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, "Baba yangu!"
Abrahamu akaitika, "Mimi hapa, mwanangu."
Isaki akasema, "Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?"
8 Abrahamu akajibu, "Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa." Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.