Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 22:6-8

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

6 Ibrahimu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaka mwanawe, naye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja, 7 Isaka akamwambia Ibrahimu baba yake, "Baba yangu!"

Ibrahimu akaitika, "Mimi hapa, mwanangu."

Isaka akasema, "Moto na kuni zipo. Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?"

8 Ibrahimu akajibu, "Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa." Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    6 Yn 19:17;1 Pet 2:24Basi Abrahamu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja. 7 Isaka akasema na Abrahamu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? 8 1 Pet 1:19Abrahamu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    6 Abrahamu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaki mwanawe, yeye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja, 7 Isaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, "Baba yangu!"

    Abrahamu akaitika, "Mimi hapa, mwanangu."

    Isaki akasema, "Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?"

    8 Abrahamu akajibu, "Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa." Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.