35 Lakini akasema, "Ndugu yako amekuja kwa udanganyifu na akachukua baraka yako."
36 Esau akasema, "Si ndiyo sababu anaitwa Yakobo? Amenidanganya mara hizi mbili: Alichukua haki yangu ya kuzaliwa na sasa amechukua baraka yangu!" Kisha akauliza, "Hukubakiza hata baraka moja kwa ajili yangu?"
Yakobo Anakimbilia Kwa Labani
41 Esau akawa na kinyongo dhidi ya Yakobo kwa ajili ya baraka ambazo baba yake alikuwa amembariki. Akasema moyoni mwake, "Siku za kuomboleza kwa ajili ya baba yangu zimekaribia, ndipo nitamuua ndugu yangu Yakobo."