Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 3:8-13

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

8 Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu katikati ya miti ya bustani. 9 Lakini Bwana Mungu akamwita Adamu, "Uko wapi?"

10 Naye akajibu, "Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha."

11 Mungu akamuuliza, "Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?"

12 Adamu akasema, "Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti, nami nikala."

13 Ndipo Bwana Mungu akamuuliza mwanamke, "Ni nini hili ambalo umelifanya?" Mwanamke akajibu, "Nyoka alinidanganya, nami nikala."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    8 Yule mwanaume na mkewe waliposikia sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka kwa Bwana Mwenyezi Mungu katikati ya miti ya bustani. 9 Lakini Bwana Mwenyezi Mungu akamwita Adamu, "Uko wapi?"

    10 Naye akajibu, "Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha."

    11 Mungu akamuuliza, "Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?"

    12 Adamu akasema, "Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa matunda ya huo mti, nami nikala."

    13 Ndipo Bwana Mwenyezi Mungu akamuuliza mwanamke, "Umefanya jambo gani?" Mwanamke akajibu, "Nyoka alinidanganya, nami nikala."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    8 Ayu 31:33;38:1;Zab 139:1-12;Yer 23:34;Amo 9:3Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. 9 Mwa 4:9BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? 10 Ayu 23:15;1 Yoh 3:20Akasema, Nilisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. 11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? 12 Mit 28:13;Yak 1:13Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. 13 2 Kor 11:3;1 Tim 2:14BWANA Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.