8 Yule mwanaume na mkewe waliposikia sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka kwa Bwana Mwenyezi Mungu katikati ya miti ya bustani. 9 Lakini Bwana Mwenyezi Mungu akamwita Adamu, "Uko wapi?"
10 Naye akajibu, "Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha."
11 Mungu akamuuliza, "Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?"
12 Adamu akasema, "Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa matunda ya huo mti, nami nikala."
13 Ndipo Bwana Mwenyezi Mungu akamuuliza mwanamke, "Umefanya jambo gani?" Mwanamke akajibu, "Nyoka alinidanganya, nami nikala."