Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 45:1-3

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Yosefu Anajitambulisha

1 Hapo Yosefu hakuweza kujizuia zaidi mbele ya wote waliokuwa wamesimama karibu naye, akapaza sauti, akasema, "Mwondoeni kila mtu mbele yangu!" Kwa hiyo hapakuwepo mtu yeyote pamoja na Yosefu alipojitambulisha kwa ndugu zake. 2 Naye akalia kwa sauti kubwa kiasi kwamba Wamisri walimsikia, hata watu wa nyumbani mwa Farao wakapata hizo habari.

3 Yosefu akawaambia ndugu zake, "Mimi ni Yosefu! Je, baba yangu angali hai bado?" Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Basi Yusufu hakuweza kujizuia tena mbele ya wote waliokuwa wamesimama karibu naye. Akapaza sauti, akasema, "Mwondoeni kila mtu mbele yangu!" Kwa hiyo hapakuwa mtu mwingine na Yusufu alipojitambulisha kwa ndugu zake. 2 Naye akalia kwa sauti kubwa kiasi kwamba Wamisri walimsikia, hata watu wa nyumbani mwa Farao wakapata hizo habari.

    3 Yusufu akawaambia ndugu zake, "Mimi ni Yusufu! Je, baba yangu angali hai bado?" Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Mdo 7:13Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze. 2 Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia. 3 Mdo 7:13;Mt 14:26;Mk 6:50Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.