Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 45

Yusufu ajitambulisha

1 Basi Yusufu hakuweza kujizuia tena mbele ya wote waliokuwa wamesimama karibu naye. Akapaza sauti, akasema, "Mwondoeni kila mtu mbele yangu!" Kwa hiyo hapakuwa mtu mwingine na Yusufu alipojitambulisha kwa ndugu zake. 2 Naye akalia kwa sauti kubwa kiasi kwamba Wamisri walimsikia, hata watu wa nyumbani mwa Farao wakapata hizo habari.

3 Yusufu akawaambia ndugu zake, "Mimi ni Yusufu! Je, baba yangu angali hai bado?" Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake.

Veja também